Thursday, 6 March 2014
HISTORIA YA ZOE
Zoe life in Christ Ministries ( LCM) ni huduma ya kinabii,Makao Makuu yake yakiwa Tabata/Segerea,Dar es salaam Tanzania.Huduma hii ilianza baada ya mtumishi wa Mungu Prophet Joseph,kuitwa na Mungu kuongoza huduma ya watu zaidi ya 70,000.Huduma ilianza miaka minne na watu watano tu.Sasa hivi inapokea zaidi ya watu 1000 kwa wiki.
LCM hatufundishi dini bali imani.tunapokea watu kutoka dini mbalimbali kama vile, Wakatoliki,Walutheri,Waislamu,Wahindi,Wayahudi na hata Wapagani wasiomjua Mungu.Tunaamini ya kwamba watu wote hawa wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na hatuna mamlaka ya kuwahukumu au kuwatenga na upendo wa Mungu ambao unafundishwa katika kanisa lake.Tunaamini kanisa ni sehemu ya kupokea kila mtu jinsi alivyo,kwani Mungu anampenda kila mtu kama alivyo.
Yeremia 29:11 maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi,asema BWANA,ni mawazo ya amani wala si ya mabaya,kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho
Ukiona wewe ni mtu mwenye dhambi karibu sana kanisani kwetu.Yesu Kristo hakuja kwa waliosafi,bali wenye dhambi ili awaokoe.(Luka 5:32),Sikuja kuwaita wenye haki,bali wenye dhambi,wapate kutubu.