TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Saturday, 18 October 2014

IBADA YA KUVUNJA KILA AINA YA NIRA

Ibada ya Jumapili hii ilikuwa ni ibada ya kuvunja nira , pale popote ambapo ibilisi amekuunganisha ni lazima pavunjwe ili uwe huru, Mungu Baba akimtumia mtumishi wake Prophet Joseph akiongozwa na Roho Mtakatifu aligawa mafuta ya Olive kwa kila aliyefika katika huduma ya LCM kwa ajili kuvunja kila nira kama alivyokuwa ameelekezwa na Baba yake wa Mbinguni. Tulishuhudia maelfu ya watu nira zikiwaacha na kuwa huru kabisa mara baada ya kupaka mafuta hayo katika paji la uso.


                     Wainjilisti wakiwa wamebeba maboksi yenye mafuta ya Olive.

                                                 Prophet Joseph akiomba.

                    Shemasi Daudi akigawa mafuta hayo kwa watu waliohudhuria ibada hii.
                         Prophet Joseph akiwa ameshikilia chupa yake ya mafuta ya Olive (Mzeituni).
          Maelfu wakipaka mafuta hayo kwenye paji la uso kama walivyoelekezwa na prophet Joseph.



Mara baada ya kupaka mafuta hayo  hivyo ndivyo ilivyokuwa maelfu wakiwa chini baada ya nira kuvunjika na kuwaacha huru kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
 Watu wakimshukuru Munguna kufurahia baada ya kuwa huru kutoka katika kila gereza la mateso. Tunakutukuza Mungu wetu kwa Ukuu wako.





H.I.V, UPOFU VYASALIMU AMRI KWA JINA LA YESU KRISTO

Ndugu John Mwakyoma kutoka Mwananyamala alipokea uponyaji kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa H.I.V kwa muda wa mika 11 na kutokuona sawasawa baada ya maombi alisikia moto ukitembea mwilini kuunguza kila aina ya vijidudu na kuwa mzima kabisa, pia hakuwa na nguvu mwilini lakini alipata nguvu hapohapo.


                               Ndugu John akishuhudia matendo makuu ya Mungu.

                      Hapa akiwa na binamu yake wakimshukuru Mungu kwa uponyaji.



                              Akimshukuru Mungu kwa kumponya magonjwa hayo yote.

YANAYOSHINDIKANA KWA WANADAMU KWA MUNGU YANAWEZEKANA.

UTASA, NGIRI VYAONDOLEWA KWA JINA LA YESU KRISTO

Ndugu Julius Hassan kutoka Mbagala alipokea uponyaji wa hernia (ngiri) na pia uume wake ulikuwa hauna nguvu baada ya maombi kila kitu kikakaa sawa na akarudi katika hali ambayo Mungu baba alimuumba nayo.
Pia Mke wake aliweza kupata neno la kinabii kutoka kwa Prophet Joseph kuwa ataenda kubeba mimba na kupata mtoto wa kike. Utukufu kwa Mungu.


                      Ndugu Julius Hassan akishuhudia matendo makuu aliyotendewa na Yesu Kristo.
                       Mke wa ndugu Julius akimshukuru Mungu kwa uponyaji wa mumewe.
                                       Prophet Joseph akiwabariki.
                                        Wakiwa chini baada ya nguvu kuwachukua.
                       Wakimshangilia Mungu kwa kuwatendea mambo makuu ya ajabu.

                                   Prophet Joseph akifurahi na ndugu Julius na mkewe.

                       Wakimtukuza Mungu sana kwa uponyaji na neno la kinabii.

Kutoka 23:26- "Hakuna atakayeharibu mimba wala atakayekuwa tasa katika nchi yako. Nami nitakupa maisha makamilifu". Kuwa na watoto ni ahadi kutoka kwa Bwana hakuna roho itakayozuia. Halleluya!!!