TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Saturday, 27 September 2014

KUKABIDHIWA WATOTO KWA MUNGU.

Jumapili hii ya tarehe 21/9/2014 ilikuwa ni siku maalum ya kuwakabidhi watoto kwa Bwana, Prophet Joseph alieleza kuwa kwenye dini wanabatiza watoto na kusema kuwa ni kinyume na Neno la Mungu, kwasababu watoto wanatakiwa wakabidhiwe kwa Mungu na si kubatizwa.

Kwa Imani watoto wanakabidhiwa kwa Mungu kama Yesu Kristo alivyokabidhiwa kwa Bwana wakati akiwa mtoto na alipofikia umri wa miaka 30 alibatizwa na Mwinjilisti Yohana Mbatizaji.
Luka 2:22 inasema Kisha, zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo torati ya Musa, Joseph na Mariam walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana. 




                                       Wazazi wakiwa na watoto wao.