Kaka huyu alijikuta akitapika baada ya nguvu ya Mungu kumchukua,akaanza kutapika sumu iliyokuwa tumboni.
Tuesday, 20 May 2014
MASS DELIVERANCE
Kaka huyu alijikuta akitapika baada ya nguvu ya Mungu kumchukua,akaanza kutapika sumu iliyokuwa tumboni.
YESU KRISTO WA NAZARETH ANAENDELEA KUUNGA MIFUPA ILIYOVUNJIKA HATA SASA...
Prophet Joseph akimuombea kwa kutumia jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Prophet Joseph akiamuru maumivu kumwachia. |
Nesi kutoka kitengo cha mifupa MOI,Mrs.Sophia Wellya akithibitisha kuwa ni kweli mfupa umeunga kwa kutumia jina la Yesu Krsisto.
Ndugu akifurahi baada ya maombezi,kwakuwa hakuwa na maumivu tena.
Nesi akielezea kuwa mfupa wa ndugu huyu umeunga kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Ndugu akielezea kuwa hana maumivu tena.
Ndugu akifurahia baada ya Mungu kumponya. |
Ndugu huyu akikanyaga chini bila ya kuwa na maumivu ya aina yoyote ile kutokana na kuombewa na Prophet Joseph kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Baada ya uponyaji ndugu wakimtukuza Mungu kwa kumponya ndugu yao.
Familia wakimtukuza Mungu kwa kumponya ndugu yao.
MGUU ULIOVUNJIKA WAUNGA NA KUPONA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH.
Katika ibada ya jumapili 18/05/2014 ndugu huyu alikuja kwenye huduma ya Life in Christ Ministries Zoe,Tabata, Segerea Dar es salaam, akiwa katika hali ya maumivu makali yaliyotokana na ajali ya kugongwa na gari akiwa anaendesha pikipiki yake,ambapo ilipelekea kuvunjika mfupa wa mguu wa kulia na kuwekea chuma ambacho kwa ripoti ya madaktari ilimpasa kwanza kuwekewa chuma hicho kisha baada ya hapo kuwekewa hogo ili kuunganisha mfupa huo lakini ndugu huyu aliamua kuja katika huduma hii ili akutane na Yesu mponyaji asiyeshindwa kuunga mfupa wowote ule. Kwa kuwa jina la Yesu Kristo lina nguvu kupita majina yote alipofika katika huduma hii Prophet Joseph akiongozwa na roho alimtolea unabii kuwa ana roho ya ajali.Alifanyiwa maombi na mfupa ukaunga kabisa,alikuja anatembelea magongo mawili na mguu wake haukuweza kukanyaga chini lakini alipoombewa aliweza kukanyaga na pia kutembelea gongo moja kutokana na chuma alichokuwa amewekewa.Hakika Mungu anashangaza sana!
Prophet Joseph akimnyoshea mkono akiamuru maumivu kumwachia kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Prophet Joseph akiamuru roho chafu ya ajali iliyosababisha mguu kuvunjika imuache kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Prophet Joseph akiamuru nguvu ya ufufuo iliyomfufua Yesu Kristo katika wafu iingie kwenye eneo ambalo mfupa umevunjika na iunge mfupa na kuweka maeneo yote ya mifupa sawa.
Prophet Joseph akiamuru kisigino kilichopinda kikae sawa kwa jina laYesu Kristo wa Nazareth.
Prophet Joseph akiamuru goti lililokuwa limekaza ambalo lilikuwa likisababisha ashindwe kukanyaga chini na kushindwa kutembea liwe sawasawa na aweze kutembea kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Prophet Joseph akimwambia ndugu huyu kuwa amepona kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth na anaweza kutembea.
Prophet Joseph akimwambia ndugu huyu simama kwasababu maumivu yameshaondolewa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth na aanze kutembea.
Ndugu huyu akianza kutembea huku maelfu wakishuhudia muujiza huu mkubwa ambao Mungu ameutenda.
Ndugu huyu akishuhudia jinsi gani Yesu Kristo amemponya. |
Ndugu huyu akimshukuru Mungu jinsi gani ambavyo Mungu amemtendea huku gongo lake likiwa limeshikwa juu na mmoja kati ya mashemasi wa Life in Christ Ministries Zoe.