TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Monday, 20 October 2014

MFUPA WAUNGA KWA JINA LA YESU KRISTO

Rajef Jetha kutoka Kunduchi alishtuka sana maana hakuwahi kuamini kuwa Yesu anaweza kuponya na kuunga mifupa lakini kwa mara ya kwanza katika maisha yake uponyaji uliomtokea yeye bila ya kushuhudiwa na mtu alikuja mkono ukiwa umefungwa na hand brace (gango) alipata ajali na kuvunjika mkono wake wa kushoto lakini alipofika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe alipokea uponyaji wake na kuwa mzima kabisa na kuamini hakika Yesu ni mponyaji.



                     Ndugu Rajef Jetha akihojiwa na mtangazaji wa Zoe Tv wakati akiingia kwenye ibada.

                         Hapa akielezea jinsi alivyopokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo.
                Shemeji yake bwana Rajef akimshangilia Mungu kwa kumponya shemeji yake.
Akiunyanyua mkono huo juu hii ni kuonyesha kuwa maumivu sio sehemu yake na haihitaji kuvaa hand brace tena.

Ahsante Yesu kwa kuendelea kutuponya.








HAKUNA CHA KUMSHINDA YESU KRISTO

Mungu wetu ni Mungu ambaye anaendelea kutenda hata sasa na hakuna ugonjwa asioweza kuuponya na wala hajaacha kuponya. Ndugu William Shija alikuja kwenye huduma ya Life in Christ Ministries Zoe akiwa na maumivu katika bega lake, maumivu hayo yalipelekea avae kitu ili kuzuia maumivu katika bega hilo. Pia miezi kadhaa nyuma alipata neno la kinaabii kutoka kwa mtumishi wa Mungu Prophet Joseph, kuwa alikuwa na roho ya kifo  na alifunguliwa kutoka katika roho ya mauti na roho ya presha na mpaka leo ndugu William anaishi akisimulia matendo makuu ya Mungu katika maisha yake.

                                Ndugu William Shija akishuhudia baada ya uponyaji.
                                 Prophet Joseph akimuombea ndugu William


                           Akiwa chini baada ya nguvu ya Mungu kumchukua.
                                   Hand Brace (gango) ikiwa chini baada ya kupokea uponyaji.
Hand Brace hiyo ikitundikwa na mmoja wa mashemasi wa huduma ya LCM Zoe kuonyesha kuwa hakika Mungu amemuweka huru ndugu William na haihitaji kuivaa tena. Utukufu kwa Mungu aliye juu!!!






UPONYAJI WAKATI WA MASS DELIVERANCE


Mass Deliverance imekuwa ya neema sana kwa utukufu wa Mungu tumeona watu wakifunguliwa kwa nguvu ya Mungu kutoka katika vifungo vya aina mbalimbali, waliokuwa hawajiwezi wameondoka wakiwa wazima kabisa.

 Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph aliziamuru roho zote chafu za magonjwa kuwaacha watu, mara tu roho chafu zilifukuzwa kwa nguvu iliyomo katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth. Ukiamini tu Yesu hawezi kukupita kamwe.



                                 Baadhi ya watu wakiwa chini baada ya roho chafu kuwaacha.


                                   Watu waliopokea uponyaji wakati wa Mass Deliverance.


                             Baadhi ya watenda kazi wa LCM wakimbeba ndugu huyu pichani.
 Jina la Yesu Kristo ni jina pekee ambalo linaweza kuwafungua watu kutoka katika vifungo vyote. Mungu tunayemtumikia sio wa kawaida.