TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Saturday, 8 November 2014

MAMIA WABATIZWA KWA MAJI MENGI

Ilikuwa ni jumatano 5/11/2014 ambayo ilikuwa ni jumatano ya neema maana mamia ya watu walipata neema ya kwenda kubatizwa kwa maji mengi na prophet Joseph, kubatizwa kwa maji mengi ni agizo kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, Mathayo 28:19- inasema;  Kwa hiyo nendeni mkawafanye watu wa mataifa yote kuwa wanafunzi wangu; mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Life in Christ Ministries Zoe tunaamini katika ubatizo wa maji mengi. Ubatizo huu ulifanyika katika ufukwe wa Bahari ya Hindi katika eneo la Kigamboni katika hoteli ya Sunrise.



                                                           Prophet Joseph .
                                        Sehemu ambapo ubatizo ulifanyika.
                          Mamia wakiwa wamewasili tayari kwa kubatizwa katika maji mengi na Prophet Joseph.
              Mamia ya watu wakisubiri kubatizwa katika maji mengi.
          
                 Prophet  Joseph akimbatiza kaka huyu kwa jina la Baba,Mwana na Roho Mtakatifu.

                      Kaka huyu akimshukuru Mungu baada ya kubatizwa kwa maji mengi.

             Nguvu za Mungu zikiwa zimemchukua kaka huyu baada ya kubatizwa.





Warumi 6:3 inasema; 
Au hamfahamu kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika kifo chake? Kwa hiyo tulikufa na kuzikwa naye kwa njia ya ubatizo ili kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka kwa wafu kwa nguvu na utukufu wa Baba, sisi pia tupate kuishi maisha mapya.

Ubatizo ni agizo la Mungu mwenyewe. UTUKUFU KWA BWANA.