Yohana 14:10, Husadiki ya kwamba mimi ndani ya Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwashauri langu; lakini baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.Watu wengi wanaaingia katika huzuni,Chuki,upweke,umaskini,magonjwa na wamejikuta hawana msaada.Mungu yupo na shetani naye yupo.Mpango wa mungu katika maisha ya kila mtu ni kuwa na afya njema,amani,furaha,upendo,kufanikiwa na kustawi katika kila jambo.Mpango wa adui ni kuchinja,kuua,na kuharibu kila jambo jema ambalo mtu anafanya.Lakini shetani anatambua kwamba hana nguvu mbele ya Mungu na anajisalimisha kwa jina la yesu kristo (Marko 1:21-28) kila jumapili watu wanawekwa huru na vifungo mbalimbali chini ya jina lenye nguvu na mamlaka la yesu kristo.Yesu kupitia mtumishi wake,Prophet Joseph anawafungua watu na vifungo mbalimbali kama kula udongo,mchele,ndoto za kufanya mapenzi,kukabwa usiku,umaskini,kuchanganyikiwa,na usagaji.
Je wewe ni jambo gani unataka Mungu akufungue limekuwa kero kwako.Kumbuka hakuna jambo gumu la kumshinda Mungu. Karibu ili Yesu abadilishe maisha yako moja kwa moja.
Thursday, 6 March 2014
UPONYAJI
Yohana 14:12 Amin,Amini, nawaambieni, yeye aniaminiaye mimi kazi nizifanyazo mimi,yeye naye atazifanya;naam kubwa kuliko hizo atafanya..."
Yesu Kristo ndiye mponyaji.LCM tunashuhudia Yesu akiwaponya watu magonjwa mbalimbali ambayo yameshindikana kama Kansa,Ukimwi,Presha,Kisukari,mifupa kuvunjika n.k. Hakuna ugonjwa ambao Mungu hawezi kuponya,kwa sababu yote yawezekana kwake.Watu wanaponywa kupitia mstari wa uponyaji "Prayer Line" na ibada nzima ya jumapili kutegemea jinsi ambavyo roho wa Mungu anavyomwongoza Mtumishi wake.Wengi wamekuja kushuhudia jinsi ambavyo Mungu amebadilisha maisha yao moja kwa moja.
Mama huyu akitoa maelezo ya tatizo lake kabla ya kuombewa na Prophet Joseph
Baada ya Maombezi
USHUHUDA-Baada ya maombezi hakika Mungu anatenda hata sasa.
Yesu Kristo ndiye mponyaji.LCM tunashuhudia Yesu akiwaponya watu magonjwa mbalimbali ambayo yameshindikana kama Kansa,Ukimwi,Presha,Kisukari,mifupa kuvunjika n.k. Hakuna ugonjwa ambao Mungu hawezi kuponya,kwa sababu yote yawezekana kwake.Watu wanaponywa kupitia mstari wa uponyaji "Prayer Line" na ibada nzima ya jumapili kutegemea jinsi ambavyo roho wa Mungu anavyomwongoza Mtumishi wake.Wengi wamekuja kushuhudia jinsi ambavyo Mungu amebadilisha maisha yao moja kwa moja.
Mama huyu akitoa maelezo ya tatizo lake kabla ya kuombewa na Prophet Joseph
Baada ya Maombezi
Ndugu huyu akiingia kwenye ibada katika kanisa la Life in Christ Ministries Zoe,aliyekuwa amepata ajali ya pikipiki na aliamini kuwa Mungu ataenda kumponya.
Akiombewa na mtumishi wa Mungu Prophet Joseph |
HISTORIA YA ZOE
Zoe life in Christ Ministries ( LCM) ni huduma ya kinabii,Makao Makuu yake yakiwa Tabata/Segerea,Dar es salaam Tanzania.Huduma hii ilianza baada ya mtumishi wa Mungu Prophet Joseph,kuitwa na Mungu kuongoza huduma ya watu zaidi ya 70,000.Huduma ilianza miaka minne na watu watano tu.Sasa hivi inapokea zaidi ya watu 1000 kwa wiki.
LCM hatufundishi dini bali imani.tunapokea watu kutoka dini mbalimbali kama vile, Wakatoliki,Walutheri,Waislamu,Wahindi,Wayahudi na hata Wapagani wasiomjua Mungu.Tunaamini ya kwamba watu wote hawa wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na hatuna mamlaka ya kuwahukumu au kuwatenga na upendo wa Mungu ambao unafundishwa katika kanisa lake.Tunaamini kanisa ni sehemu ya kupokea kila mtu jinsi alivyo,kwani Mungu anampenda kila mtu kama alivyo.
Yeremia 29:11 maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi,asema BWANA,ni mawazo ya amani wala si ya mabaya,kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho
Ukiona wewe ni mtu mwenye dhambi karibu sana kanisani kwetu.Yesu Kristo hakuja kwa waliosafi,bali wenye dhambi ili awaokoe.(Luka 5:32),Sikuja kuwaita wenye haki,bali wenye dhambi,wapate kutubu.