Akishuhudia jinsi alivyopokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo.
Akitembea bila ya kuwa na maumivu yoyote.
2. Tekla Kameta kutoka Madale alikuwa akisumbuliwa na ganzi katika magoti yake, hakuweza kutembea pasipo msaada wa fimbo lakini kwa uaminifu wa Mungu alipokea uponyaji wakati wa kipindi cha kufunguliwa kwa pamoja. Utukufu kwa Mungu.
Ndugu Tekla akiingia katika nyumba ya Mungu, LCM.
Akitembea mwenyewe baada ya maombi.
Akitembea bila ya msaada wa kifaa cha kutembelea.
3.Ndugu Arifu Hosa kutokea Gongo la Mboto jijini Dar es salaam, miaka mitatu iliyopita alipata ajali ya gari na kusababisha mguu wake kuvunjika, madaktari wakamwekea chuma mguuni ili kuunga mfupa wakena kusababisha atembelee fimbo ili kumsaidia kutembea. Lakini mguu uliendea kupata maumivu makali na kidonda hakikupona. Kwa utukufu wa Mungu jumapili ya tarehe 11/1/2015 alifika katika nyumba ya Mungu Life in Christ Ministries Zoe na hakika Mungu hakumwacha arudi kama alivyokuja. Katika kipindi cha cha Mass deliverance (kufunguliwa kwa pamoja) wakati Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alipokuwa akiamuru mifupa iunge ndugu Arifu mfupa uliunga pale pale.
Mara baada ya kupokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.
Akimshukuru Bwana Yesu kwa kumweka huru kutoka katika roho ya maumivu.
Fimbo ikiwa chini, hii ni kuonyesha kuwa kutembelea fimbo si sehemu ya maisha yake.
Akishuhudia matendo makuu ya Mungu.
Maumivu yakiwa yamemwacha akitembea huku akimshukuru Mungu.
Hakika Jina la Yesu Kristo ni Jina lipitalo majina yote!!!.