Ibada imekwisha kuanza katika nyumba ya Mungu, LIFE IN CHRIST MINISTRIES. Kwahiyo ni vema tukaanza pamoja Prophet Joseph ameingia na kuanza kusoma Mwanzo 18:14 ambayo inasema" kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA?" Pindi aliposoma tu neno hili tumeona nguvu ya Mungu ilianza kuponya watu na kuwafungua watu mbalimbali, kuna watu waliofika wakiwa hawawezi kutembea lakini kutokana na kuamini neno la Prophet ambaye ametumwa na Mungu mwenyewe, watu walipokea uponyaji hapohapo, hakika Mungu wetu anaendelea kutenda na ni mshindi na hajawahi kushindwa hata siku moja.... HALELUYA KWA BWANA.
Watu waliokuwa wamechukuliwa na nguvu ya Mungu.
Ndugu aliyekuwa hawezi kutembea akiwa anatembea baada ya kuamini neno la Mungu liliongozwa na Prophet Joseph.
Mama huyu akiwa ameweza kutembea kwa nguvu ya neno la Mungu.
Mama huyu akiwa ameweza kutembea bila ya kutumia fimbo.
Kaka huyu aliyekuwa na maumivu makali ya mguu kwa miaka 3 baada ya kusikia neno la Mungu akawa mzima na kuweza kutembea.