TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 21 September 2014

APOKEA UPONYAJI WA KITOVU KUTOKA KWA YESU KRISTO

Kaka yetu alikuwa na matatizo yaliyodumu kwenye mwili kwa muda mrefu, hasa kwenye kitovu chake hii ilisababishwa na alipokuwa mdogo wazazi wake kuchukua kitovu chake kwa mambo ya kimila kwasababu wazazi wake ni waabudu mizimu. Lakini alipokutana na Yesu mfungua vifungo aliweza kuwa huru kabisa mbali na kuonewa na ibilisi.

                   Prophet Joseph akiamuru kila roho iliyoshikilia kitovu chake kumwachia.



                            Tunaona roho hiyo chafu ikimwacha kaka huyu.
                                 Baada ya kuwa huru akimshukuru Mungu.


                           Kila roho chafu inasalimu amri kwa jina la Yesu Kristo.

APOKEA UPONYAJI WA KIFUA NA SIKIO

Dada Catherine Mathew alikuja akiwa anasumbuliwa na matatizo ya kifua yaliyopelekea ashindwe kupumua vizuri na pia alikuwa na tatizo la kutokusikia vizuri kwa muda mrefu hakuweza kusikia kitu chochote kwa kutumia sikio hilo, lakini wakati mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alipoamuru kila minyororo ya ugonjwa iliyomshikilia mtu imwachie ndipo  dada Catherine aliweza kupokea uponyaji wake wa kifua na sikio hapo hapo.

                    Akieleza jinsi ambavyo alikuwa anasumbuliwa na magonjwa hayo.
Hapa tunaona akiwa ameziba sikio lake la kulia na Prophet Joseph akimwongelesha kwa mbali na yeye alisikia bila ya tatizo lolote,hii ni baada ya maombi.
Hapa akihema bila ya kuwa na matatizo ya kifua tena. Matatizo ya  kifua na sikio yakawa ni historia katika maisha yake.

Ahsante Yesu kwa kuendelea kuwaponya watu wako.

MAUMIVU YA MUDA MREFU YAONDOLEWA NA YESU MTENDA MIUJIZA

Dada Fatma Victor alikuja akiwa na maumuvu  katika upande wa kulia yaliyodumu kwa miaka 3 na alikuwa akihisi mwili wake kuwa ni mzito pia alikuwa akishindwa kujigeuza akiwa kitandani kutokana na maumivu hayo aliyokuwa nayo. Lakini mara baada ya maombi yaliyoongozwa na Prophet Joseph dada huyu alipokea uzima kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.

     Hapa akionyesha jinsi ambavyo anaweza kugeuka bila ya kuwa na maumivu ya aina yoyote.
                     Hapa akijibonyeza kuonyesha kuwa roho ya maumivu imeondolewa.


KUSIFU KUNAWAPASA WANYOFU WA MOYO...

Baadhi wa maelfu waliofika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe ,wakimwabudu Mungu ,wakiwa wanaongozwa na Zoe Worship Team,huku wakitafakari ukuu na uweza wa Mungu ishara,maajabu na miujiza ilionekana.

Zoe Worship Team.



Sifa na Utukufu ni kwa Mungu aliye juu!!! Mungu wa Ibrahimu,Isaka na Yakobo.

APOKEA UPONYAJI WAKATI WA MAOMBI YA PAMOJA.

Mama yetu Margret kutoka Tabata alikuwa na maumivu katika mguu wake wa kushoto kuanzia alipokuwa na umri wa miaka 14 na alipokwenda hospitalini aliambiwa kuwa ana matatizo ya ugonjwa wa moyo, alikuwa akipata maumivu makali yalipelekea hata ashindwe kugeuka akiwa kitandani na pia alikuwa na maumivu ya bega lakini baada ya maombi yaliyoongozwa na Prophet Joseph kwa kutumia jina la Yesu Kristo alipokea uponyaji na kuwa mzima kabisa...