TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Saturday, 2 May 2015

MFUPA ULIOVUNJIKA WAUNGA PAPO HAPO KWA NGUVU ZA MUNGU

Fredrick Daniel alifika katika nyumba ya Mungu akiwa na hogo mkononi mwake kutokana na jali ya pikipiki aliyopata, kutokana na ajali hiyo mfupa katika mkono wake ulivunjika. Mtumishi wa Mungu prophet Joseph alimwombea kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth na mfupa uliunga papo hapo, awali hakuweza kupiga makofi wala kubeba vitu vizito lakini mara baada ya maombi aliweza kufanya yote hayo kwa neema ya Mungu.

                                   Ndugu Fredrick akiwa kwenye nyumba ya Mungu LCM ZOe.


                                               Akielezea jinsi alivyoumia mkono huo.
 Akitoa kifaa hicho maalum kilichokuwa kinamsaidia, baada ya maombi kutoka kwa prophet Joseph. Aliamuriwa akitoe kwa jina la Yesu Kristo maana maumivu yalishamwacha. 

                                                            Cheti cha hospitali.

                                   X-ray inavyoonyesha jinsi mfupa ulivyokuwa umevunjika.
 Mara baada ya maombi aliweza kunyosha mkono juu awali hakuweza kufanya kutokana na maumivu makali aliyokuwa nayo.

 Afisa muuguzi wa huduma akikagua mkono wa ndugu Fredrick kuonyesha ni kweli Yesu ametenda.
                                              Akinyanyua kiti bila ya kuwa na maumivu.
 Kifaa hicho kaka Fredrick akiwa amekitupa kuonyesha kuwa hakihitaji tena katika maisha yake.
                               Afisa muuguzi akiondoa hogo kwenye mkono wa ndugu Fredrick.
                           Hogo likiwa limekatwa na kutupwa maana si sehemu ya maisha yake.

                                            Akimtukuza Mungu kwa kumponya.

                                                    YESU ANATENDA HATA SASA!






MIRIJA YA UZAZI ILIYOZIBA YAZIBUKA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Haijalishi mirija imeziba au madaktari wamesema nini juu yako kwa nguvu na uweza wa Mungu hakuna linaloshindikana. Ndivyo ambavyo ilikuwa kwa ndugu Esau Mbilinyi na mke wake, hakika walikuwa na kila sababu ya kumtukuza Mungu kwa jinsi alivyowatendea katika maisha yao. 
Walikuwa wamekata tamaa mara baada ya kuhangaika kutafuta mtoto kwa zaidi ya miaka 5 bila ya kupata suluhisho, ndipo walipoamua kulileta tatizo hilo mbele ya Yesu Kristo mtenda miujiza. Walifika katika nyumba ya Mungu L.C.M Zoe kutokana na tatizo la kuziba mirija yote miwili ya uzazi ya Mrs. Esau Mbilinyi haikuwa rahisi kwa Mrs. Esau kuweza kubeba ujauzito kutokana na mirija hiyo kuziba.
Mwaka 2014 walifika na kupita kwenye mstari wa maombezi ( prayer line) mtumishi wa Mungu prophet Joseph aliwaombea na kuwauliza idadi ya watoto wanaotaka mara baada ya maombi walirudi nyumbani na kukutana kama mke na mume, hakika Mungu anajibu kama ukiamini waliamini na hakika Mungu aliwatendea.
Siku ya kujifungua ilipofika madaktari walipanga kumfanyia oparesheni lakini kwa neno la imani kutoka kwa mtumishi wa Mungu Prophet Joseph hawakuweza kumfanyia oparesheni na alijifungua kawaida pasipo kupasuliwa, mnamo saa 9 za alfajiri alijifungua mtoto wa kike mwenye afya tele. Kuwa na watoto ni ahadi ya Mungu kwetu sisi.

                                               MR. NA MRS ESAU MBILINYI.
                                X-RAY IKIONYESHA MIRIJA ILIVYOKUWA IMEZIBA.
 HUYU NDIYO MTOTO WA KIKE MWENYE AFYA TELE ALIYEZALIWA KWA MAOMBI.
                      VYETI VYA HOSPITALI KIKIONYESHA VIPIMO VYA MRS. ESAU.

 Kumbukumbu la Torati 7:14 inasema ; Utabarikiwa kuliko mataifa yote; hakutakuwa na mtu mume wala mke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu wa mifugo.

                                          SIFA NA UTUKUFU KWA BWANA.