Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kazi,Ajira na maendeleo ya Vijana Dkt. Milton Mahanga aliweza kupokea uponyaji katika mstari wa uponyaji ( Prayer line) katika ibada ya Jumapili 2/11/2014, alikuja akiwa na maumivu ya miguu lakini alikutana na Yesu Kristo mponyaji naye akaponywa na kuwa huru kabisa.
Dkt. Milton Mahanga akiwa katika mstari wa uponyaji.
Prophet Joseph akimuombea Dkt. Mahanga kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Roho ya maumivu ikifukuzwa kwa jina la Yesu Kristo.
Hakika Mungu hashindwi na jambo lolote, hapa tunaona Mh. Mahanga akimshangilia Mungu baada ya maumivu kumwacha.
SIFA NA UTUKUFU NI KWA YESU KRISTO.
Sunday, 2 November 2014
PINGILI ZA MGONGO ZAKAA SAWA KWA JINA LA YESU KRISTO
Mheshimiwa Ritha Mlaki mbunge viti maalum katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuja akiwa na tatizo la kupishana kwa pingili za mgongo kuanzia mwaka 2002 ambayo ilipelekea maumivu katika goti na mkono wake wa kulia na hakuwa anaweza kutembea sawasawa na ilibidi avae lumbar corset ili kupunguza maumivu. Alipokea uponyaji katika ibada ya Mass Deliverance iliyoongozwa na Prophet Joseph akiongozwa na Roho Mtakatifu, mara baada ya maombi hayo alipokea uponyaji hapo hapo kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareth na kuwa mzima kabisa. UTUKUFU KWA YESU KRISTO.
Kabla ya maombi akiwa amevaa lumbar corset hiyo.
Mh. Ritha Mlaki akiwa mwenye furaha baada ya kupokea uponyaji.
Akiwa ni mwenye furaha tele baada ya maumivu kumwacha.
Mh. Ritha Mlaki akishuhudia jinsi alivyopokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo pembeni ni msaidizi wake.
Akitembea bila ya kuwa na maumivu yoyote.
Akikunja mguu kuonyesha kuwa maumivu yamemwacha kwa Jina la Yesu Kristo.
Lumbar corset ikiwa chini baada ya kupokea uponyaji .
Akimshukuru Mungu kwa kupokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.
SIFA NA UTUKUFU NI KWA YESU KRISTO.
Kabla ya maombi akiwa amevaa lumbar corset hiyo.
Mh. Ritha Mlaki akiwa mwenye furaha baada ya kupokea uponyaji.
Akiwa ni mwenye furaha tele baada ya maumivu kumwacha.
Mh. Ritha Mlaki akishuhudia jinsi alivyopokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo pembeni ni msaidizi wake.
Akitembea bila ya kuwa na maumivu yoyote.
Akikunja mguu kuonyesha kuwa maumivu yamemwacha kwa Jina la Yesu Kristo.
Lumbar corset ikiwa chini baada ya kupokea uponyaji .
SIFA NA UTUKUFU NI KWA YESU KRISTO.
TAZAMA ILIVYO VYEMA NA KUPENDEZA NDUGU WAKAE PAMOJA KWA UMOJA....
Katika ibada ya jumapili 2/11/2014 tuliweza kupata neema ya kutembelewa na viongozi wa siasa wawili nao ni Dkt Milton Makongoro Mahanga, naibu Waziri wa Kazi,Ajira na maendeleo ya Vijana na pia ni mbunge wa jimbo la Tabata jijini Dar es salaam, Pamoja na Mh. Ritha Mlaki mbunge viti maalum.
Walifika katika huduma ya LCM kuabudu pamoja nasi lakini pia kupata uponyaji wao kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.
Mh. Milton Makongoro Mahanga na Mh. Ritha Mlaki .
Walifika katika huduma ya LCM kuabudu pamoja nasi lakini pia kupata uponyaji wao kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.
Mh. Milton Makongoro Mahanga na Mh. Ritha Mlaki .
NGUVU YA UFUFUO KATIKA JINA LA YESU KRISTO
Dada Brenda kutokea Tabata jijini Dar es salaam ana kila sababu ya kushuhudia kwa matendo makuu ambayo Mungu amemtendea katika maisha yake, Brenda alikuwa aanasumbuliwa na ugonjwa wa sickle cell kwa muda mrefu alipelekwa hospitalini na kutibiwa lakini ugonjwa huo haukumwacha na hali yake ilizidi kuwa mbaya. Ndipo ndugu yake alipoamua kumleta katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe iliyopo Tabata Segerea ili Yesu mtenda miujiza awatendee, walifika majira ya saa 9 alfajiri, alifika akiwa katika hali ya umauti kabisa maana alishakata tamaa kama anaweza kuishi tena.
Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph, akamwombea na kuifukuza roho ya kifo na sickle cell kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth ndani ya Brenda, naye akapokea uzima na kuwa huru mbali ya kuonewa na Ibilisi.
Hapa akiwa mzima baada ya kuombewa na Prophet Joseph kwa jina la Yesu Kristo.
Prophet Joseph akimpa maelekezo ya jinsi gani aendelee kutunza uponyaji wake.
Hapa akionekana mwenye nguvu maana hakuweza kutembea alikuja akiwa amebebwa lakini mara baada ya kupokea nguvu ya ufufuo anatembea mwenyewe.
Akishuhudia jinsi Mungu alivyomponya na kumtoa katika roho ya kifo.
Ndugu yake aliyemleta akimshukuru Mungu kwa aliyowatendea.
Brenda akitokwa na machozi ya furaha baada ya kurejeshewa uhai na Yesu Kristo wa Nazareth.
Hakika kuna nguvu ya ufufuo katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa Facebook ambao ni Life in Christ Ministries Zoe.