TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 9 November 2014

SHUHUDA ZA MASS DELIVERANCE

1.Dada Dili alikuja akiwa na maumivu kwenye pua yake hakuweza hata kuingiza kidole kwenye pua kutokana na maumivu makali aliyokuwa nayo lakini baada ya maombi ya Mass deliverance,alipokea uponyaji na kuwa mzima kabisa. Utukufu kwa Bwana.


                               Dada Febronia akishuhudia matendo makuu ya Mungu.
                       Miwani ikiwa chini kuonyesha ishara ya kuwa ni mzima kwa jina la Yesu Kristo.
Akiiweka kwenye ukuta wa uponyaji ikiwa na maana haihitaji tena kuvaa miwani.

2. Febronia Temanyika alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kichwa kwa zaidi ya miaka 20 na ilimpelekea avae miwani na pia hakuweza kutembea kwenye jua kali mtumishi wa Mungu,Prophet Joseph alipoamuru maumivu yote ya kichwa kuwaacha watu dafa Febronia alipokea uponyaji wake hapo hapo na kuwa mazima kabisa. Jina la Bwana litukuzwe.

3. Mama Renatha alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya mabega na mkono wake ulikuwa unapata ganzi na hakuweza kunyosha mkono huo,baada ya maombi ya Mass Prayer alipokea uponyaji na kuwa mzima kabisa. Pia alipata neema ya kupata shilingi laki moja 100,000/= pesa taslimu kutoka kwa mtumishi wa  Mungu, Prophet Joseph.


                                     Akishuhudia jinsi ambavyo amepokea uponyaji wake.
                                                  Prophet Joseph akiwa na mama Renatha.
                                     Mwinjilishi Andrew akimkabidhi mama Renatha pesa hizo.

                          Prophet Joseph akimshukuru Mama Renatha kwa kupokea pesa hizo .

                                       UTUKUFU KWA BWANA WETU YESU KRISTO.




MATENDO MAKUU YA MUNGU.....

Hakika Mungu ni mwema kila siku tumeendelea kumwona Mungu akifungua watu kupitia mtumishi wake Prophet Joseph,watu waliokuja na vifungo Yesu Kristo amewafungua nao wako huru moja kwa moja.

   Baadhi ya watu wakiwa chini baada ya nguvu ya Mungu kuwashukia na kufukuza nguzu za adui ndani yao.

                               Mama huyu akitapika kila aina ya sumu iliyokuwemo ndani yake.
                                                       Kaka huyu akitapika kila aina ya sumu.
                 Hawa ni baadhi ya maelfu ambao walifunguliwa katika ibada ya Mass deliverance.