TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Thursday, 15 January 2015

MGUU ULIOVUNJIKA WAUNGA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Fredy Chengula kutokea Kimara alipata ajali ya pikipiki na kupelekea mguu wake kuvunjika, alipokwenda hospitalini madaktari walimwekea chuma katika mguu wake. Lakini wakati wa maombi ya kufunguliwa kwa pamoja mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph alipoamuru mifupa kuunga kw ajina la Yesu Kristo ndugu Fredy mfupa uliunga na maumivu yakamwacha kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.


                                      Ndugu Fredy akiingia katika nyumba ya Mungu LCM.
                                                              Akitembelea gongo.
                                             Akiwa amekaa ndani ya nyumba ya Mungu.
                 Mara baada ya kupokea uponyaji, akitembea bila ya msaada wa gongo.
                                      Akionyesha jinsi mguu wake ulivyokuwa umeshonwa.

Bwana wetu Yesu Kristo anaendelea kuunga mifupa hata sasa! Sifa kwa Yesu Kristo mtenda miujiza.


KUFUNGULIWA KWA PAMOJA

Zaburi 107:20- inasema " Hulituma neno lake na kuwaponya, akawaokoa kutoka maangamizo". Baada ya mtumishi wa Mungu Prophet Joseph kufundisha somo linalosema MAISHA YA MUNGU TULIYONAYO  ikafuatia na kipindi cha kufunguliwa kwa pamoja ( Mass Deliverance) na maisha ya Mungu (ZOE) yakaingia ndani ya watu kufukuza kila aina ya udhaifu na magonjwa. Hakika tulimuona maisha ya Mungu yakiingia ndani ya watu na watu kufunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali. Hii ni katika ibada ya tarehe 11/1/2015.


                     Baadhi ya watu waliofunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali.

                           Nguvu ya Mungu ikifukuza kila aina ya uonevu wa shetani ndani ya watu.



MAUMIVU MAKALI YA TUMBO YAMWACHA MOJA KWA MOJA


Lucy Godfrey kutoka Pugu jijini Dar es salaamaliletwa hapa katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe  siku ya Alhamisi ya tarehe 8/ 1/2015 akiwa na maumivu makali ya tumbo yaliyopelekea ashindwe kula,kukaa na hata kulala. Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph hakuwepo wakati dada huyu alipoletwa.
Alitoa maelekezo kupitia simu kwa mmoja kati wa wainjilisti kuwa dada huyu apewe maji ikiwa ni maelekezo kutoka wa Roho Mtakatifu akimwongoza Prophet Joseph. Mara tu alipopewa maji aliweza kusimama na kutembea  na kufany akila lililokuwa linamshinda kufanya kabla ya maombi. Wakati Lucy akinywa maji hayo jambola kushangaza lilitokea nguvu ya Mungu ilimchukua dada Neema, Neema ndiye aliyemleta Lucy. 



                                      Lucy akionekana akiwa amejilaza kwnye gari.

                              Dada Neema akihojiwa na mtangazaji/ mwinjilisti Joyce wa Life Zoe Tv.
 Mmoja wa wainjilisti, mwinjilisti Juliana akiwa na maji ya kunywa kama alivyopewa maelekezo na Prophet Joseph.
                                          Dada Lucy akinywa maji hayo.
                                    Nguvu ya Mungu ikiwa imemchukua dada Neema.
            Hapa dada Lucy ni mara baada ya kunywa maji akiwa ni mzima kabisa.
                 Maumivu yakiwa yamwemwacha akijinyosha kuonyesha kuwa hana maumivu tena.
                                                             Akilia machozi ya furaha.

                 Hakika neno la Nabii likiwa limevuviwa na Roho Mtakatifu lazima litende miujiza.
                                        Dada Lucy aliondoka akiwa ni mzima kabisa.
                                                                  Haleluya!!!




ASTHMA YAONDOLEWA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Sasha Kapinga aliletwa na mama yake Saida Kapinga katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe kwasababu ya tatizo la pumu, Sasha alikuwa akisumbuliwa na pumu kuanzia alipokuwa na umri wa miezi 7 na hadi sasa ana miaka 5 , walienda nchini Afrika ya Kusini zaidi ya mara saba lakini hali haikubadilika. Ndipo alipoamua kutafuta msaada wa Mungu, walifika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe kwa maombi jinsi Mungu wetu alivyomwaminifu, Mungu alimgusa mtoto Sasha katika prayer line na kuwa mzima kabisa kutoka katika mateso ya kuumwa pumu.

                                                     Sasha akiwa na mama yake.
                                            Saida Kapinga akielezea hali ya mtoto wake.
                                Akionyesha dawa anazotumia Sasha hii ni kabla ya maombi.
                                                      Dawa zinavyoonekana pichani.

  Mama yake Sasha akionyesha jinsi ambavyo hutumia dawa hizo kwa mwanaye kila siku .
                       Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph akifukuza roho ya pumu katika jina la Yesu Kristo ndani ya  Sasha. Sifa na Utukufu ni kwa Bwana wetu Yesu Kristo.








APOKEA UPONYAJI KATIKA IBADA YA MASS DELIVERANCE

Hakika Mungu wetu anashangaza sana yaliyoshindikana kwa wanadamu kwake Mungu yanawezekana. Jenipher Everest alipata ajali mwezi wa 3 mwaka jana, ajali amnayo ilisababisha mguu wake kuvunjika alikwenda hospitali na akafanyiwa oparesheni tatu lakini mguu haukuunga na akawa akitumia gongo kutembea, alirudi tena katika hospitali ya Regency na akapewa ushauri na madaktari kuwa inabidi aende nchini India kwa matibabu zaidi lakinikwa neema ya Mungu alikutana na mtu aliyemwelekeza katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe jumapili hiyo alifika katika huduma ya LCM Zoe na Mungu hakumwacha alipokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.

                                            Dada Jenipher akitembea kwa msaada wa fimbo.
                                         Prophet Joseph akifukuza kila roho ya maumivu.
                                             Akitembea bila ya msaada wa fimbo.
                          Fimbo ikiwa juu kuonyesha kuwa hakika amepokea uponyaji.
                                           Akishuhudia matendo makuu ya Mungu.
                                       Akikanyaga chini bila ya kuwa na maumivu yoyote.

                 Akitembea bila ya msaada wa fimbo, hakika Mungu anatenda hata sasa.

                                                 Utukufu ni kwa Mungu mwenye uwezo...