TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Saturday, 29 November 2014

MAELFU WALIOFUNGULIWA KUTOKA KATIKA VIFUNGO MBALIMBALI

Hawa ni baadhi tu  ya maelfu waliofunguliwa kutoka katika vifungo vya kula mchele,makaratasi,barafu,mkaa,chaki,mifuko ya plastiki na vitu vingi vichafu lakini kwa upendo wa Mungu wetu waliwekwa huru na Yesu Kristo na hapa wakishuhudia toka wamefunguliwa hawana hamu ya kula tena vitu hivyo vichafu.



Baadhi tu ya waliofunguliwa kutoka katika kifungocha kula vitu vichafu. Sifa kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

KWA HABARI ZAIDI TEMBELEA UKURASA WETU WA FACEBOOK LIFE IN CHRIST MINISTRIES ZOE. AHSANTENI.

SHUHUDA


Maelfu walishuhudia na kumshukuru Mungu jinsi ambavyo amewatoa katika vifungo vya ulevi na uvutaji sigara wa muda mrefu.


                                    Yanayoshindikana kwa wanadamu kwa Mungu yanawezekana.

AFUNGULIWA KUTOKA KATIKA KIFUNGO CHA MUME WA KIPEPO (SPIRITUAL HUSBAND)

Mungu ni mwenye upendo na rehema sana kwetu dada Neema Mbajo alikuwa katika mateso ya muda mrefu kuanzia akiwa katika kidato cha tatu alikuwa akiota anafanya mapenzi na mwanaume asiyemfahamu, ikafikia hatua akawa akimuona mwanaume huyo kinadharia, yaani mwanaume huyo alikuwa akimtokea bila ya kuota. Siku moja akiwa anatembea njiani ndege wawili walikuja na kutua kichwani kwake na kuanza kupigana mara akaanguka na kuzimia alikwenda sehemu nyingi lakini hakupata msaada. Alipomaliza shule aliolewa lakini kutokana na kuwa na mume wa kipepo ndoa yake iliharibika. Pia alijaribu kufungua biashara mbalimbali lakini hazikufanikiwa kutokana na mume huyu wa kipepo kumuharibia biashara na maisha yake. Alipofika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe, Yesu Kristo mtenda miujiza alimfungua kwa kupitia mtumishi wake Prophet Joseph na kuwa huru  kabisa kutoka katika mateso ya muda mrefu.

                                              Akielezea jinsi roho hiyo chafu ilivyomtesa.

Hakuna jambo gumu la kumshinda Yesu, yeye ni Alfa na Omega ( ni mwanzo tena mwisho)                                                             Utukufu kwa Yesu Kristo.

USHUHUDA WA MASS DELIVERANCE

Leticia Musore kutoka Tabata alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya mbavu,kifua,kiuno na miguu, Alifika kushuhudia jinsi Yesu Kristo wa Nazareth alivyomponya, wakati wa mass deliverance mtumishi wa Mungu Prophet Joseph aliamuru kukataa magonjwa mama huyu pindi alipokataa magonjwa aliwekwa huru na Yesu Kristo na maumivu yote yakamwacha kwa jina la Yesu Kristo.

Akishuhudia jinsi ambavyo Yesu Kristo amemponya na kumfungua kutoka katika kifungo cha roho ya maumivu. Ahsante Yesu Kristo.






MKONO WAUNGA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Mama huyu alifika akiwa amefungwa POP mkononi, sababu iliyopelekea kufungwa na POP ni kwamba akiwa nyumbani kwake alisikia kizunguzungu  na kuanguka chini alipoanguka alivunja vidole vyake vya mkononi. Lakini kwa Neema ya Mungu alipofika katika ibada ya jumapili 23/11/2014 alipokea uponyaji wake mara moja kutoka kwa Yesu Kristo.



                             Mama huyu akiingia katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe.


                              Akinyoosha mkono juu bila ya kuwa na maumivu yoyote yale.
            Afisa wa afya kutoka katika Hospital ya wilaya Temeke akikagua mkono wa mama huyu na kuthibitisha kuwa ni kweli mama yetu amepokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo.
                           Mama huyu akimshukuru Mungu kwa kumponya mkono wake....

                                                  HAKIKA YESU ANAWEZA.

NGUVU YA UPONYAJI KATIKA JINA LA YESU KRISTO

Kuna nguvu ya uponyaji katika jina la Yesu Kristo, haijalishi tatizo linalokusumbua ukiamini kuwa Yesu Kristo anaweza kukuponya hakika atakuponya. Mama huyu alikuja akiwa na maumivu katika mguu wake uliopelekea kupata kidonda kikubwa katika mguu huo lakini aliamini kuwa hakika Yesu Kristo atamponya wakati wa maombi ya Mass deliverance mtumishi wa Mungu Prophet Joseph aliamuru roho za maumivu na magonjwa kuwaacha watu kwa jina la Yesu Kristo ndipo mama huyu akapokea uponyaji wake.


                                                           Mguu huo unavyoonekana.

MAGONGO YATUPWA KWA JINA LA YESU KRISTO

Atupele kutoka Mafinga, Iringa alikuwa na maumivu makali katika mguu wake na kusababisha ashindwe kutembea pasipo msaada wa magongo. Madaktari walimweleza kuwa mfupa wake wa mguu umepishana. Lakini wakati wa Mass deliverance iliyoongozwa na Prophet Joseph mama huyu aliweza kutembea bila ya msaada wa magongo. Hakika Mungu ni mwema sana.


                                   Mama huyu  akitembea bila ya msaada wa fimbo.
                                              Akishuhudia matendo makuu ya Mungu.

Gongo hilo likiwa limeshikwa juu na mmoja wa watenda kazi katika huduma hii ya Life in Christ Ministries Zoe, ikionyesha kuwa mama huyu ni mzima na haihitaji kutembelea gongo tena. UTUKUFU KWA BWANA WETU YESU KRISTO.