TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Thursday, 19 February 2015

SHUHUDA ZA KUPONA MFUPA ULIOVUNJIKA

Mary Ligola kutokea Kibamba alikuja wiki iliyopita akiwa na P.O.P mkononi mara baada ya kuvunjika mfupa katika mkono wake kwa neema ya Mungu alipokea uponyaji wake na mkono kuunga papo hapo, jumapili ta tarehe 15/2/2015 alikuja kushuhudia kuwa toka siku aliyopokea uponyaji hadi hivi sasa yeye ni mzima kabisa.


           Hivi ndivyo Mary Ligola alivyokuwa katika ibada ya jumapili tarehe 8/2/2015

                          Kwa utukufu wa Mungu hivi ndivyo anavyoonekana sasa.


                        Mama mzazi wa Mary akimtukuza Mungu kwa kumponya binti yake.
                   Mary akipunga mkono ikionyesha kuwa hakika mfupa uliunga siku ile ile.

                                    Utukufu kwa Mungu mwenye uweza wote.






MFUPA WA MKONO ULIOVUNJIKA WAUNGA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Twalibu Yusuph kutoka Bunju - Dar es salaam alipata ajali ya kuvunjika mfupa wa mkonowakati akiwa kwenye shughuli zake za ujenzi, mkono huo ulikuwa ukimpa maumivu makali kwa neema ya Mungu alipokea uponyaji wa mkono kuunga papo hapo.

                             Ndugu Twalibu akiingia kwenye nyumba ya Mungu, ZOE LCM.
                                                            Akisikiliza neno la imani 

               Prophet Joseph akiamuru mkono huo kuunga kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
                     Mara baada ya maombi akimwelekeza ndugu Twalibu kuukunja mkono huo.
 Prophet Joseph akiondoa kamba iliyokuwa imeshikilia hogo kwenye mkono wa ndugu Twalibu.
               Ndugu Twalibu akinyanyua mkono juu bila ya kuwa na maumivu ya aina yoyote ile.

 Afisa muuguzi kutoka katika wilaya ya Temeke akithibitisha kuwa ni kweli mkono huo umeunga.
                      Hivi ndivyo mkono huo ulivyokuwa ukionekana wakati ukiwa na hogo.
Akipiga makofi bila ya kuwa na maumivu ya aina yoyote hakika Yesu Kristo bado anaunga mifupa hata sasa, ukiamini kila kitu kitaponywa hakuna ugonjwa asioweza kuponya.





MFUPA WA MGUU WAUNGA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH


Charles Mduma kutoka Katavi, Sumbawanga alipata ajali ya kugongwa na pikipiki wakati akiingia kwenye gari lake pikipiki ilikuja na kumgonga na kusababisha mfupa katika mguu wake kuvunjika, alikwenda hospitalini na kuwekewa hogo ambalo alitakiwa akae nalo kwa muda kisha arudi hospitalini ili awekewe chuma. Lakini yanayoshindikana kwa wanadamu kwa Mungu yanawezekana, mara baada ya kusikia neno la uzima na lenye nguvu ya kuponya kila aina ya ugonjwa ndugu Charles alipokea uponyaji wa mguu wake.


                              Ndugu Charles akiingia kwenye nyumba ya Mungu, Zoe LCM.



                                           Prophet Joseph akimhoji juu ya mguu huo.

 Prophet Joseph akiamuru uponyaji  kuingia na mfupa huo kuunga kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.



                                             Akitembea bila ya msaada wa magongo.
                                 Akiliondoa hogo hilo mara baada ya kupokea uponyaji.
 Mmoja kati ya wainjilisti wa Zoe LCM akisaidia kuondoa hogo kwenye mguu wa ndugu Charles.
                  Akilivua hogo hilo mara baada ya kulikata maana si sehemu ya maisha yake.
     Akiwa ni mwenye furaha mara baada ya kupokea uponyaji na mfupa kuunga kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.



HAKIKA MUNGU WETU ANATENDA HATA SASA

Wakati wa ibada ya mass deliverance (kufunguliwa kwa pamoja) ya tarehe 15/2/2015 Mungu aliendelea kuwafungua watu wake kutoka katika vifungo mbalimbali kwa kumtumia mtumishi wake prophet of God, prophet Joseph. Maelfu walifunguliwa kutoka katika kila uonevu wa ibilisi na kila mateso yaliwaacha watu na kuwa huru katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth.

Hawa ni baadhi ya maelfu ya waliopokea uponyaji wao wakati wa Mass deliverance.


1. Sophia Daudi amepokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth, kutoka kwenye maumivu makali ya tumbo na kiuno na pia alikuwa akitokwa na damu kwa wiki mbili mfululizo. Mara baada ya maombi ya kufunguliwa kwa pamoja alipokea uponyaji wake papo hapo na alipokwenda kujikagua akajikuta damu imekata kabisa.

2. Mary Nyoni kutoka Tabata alikuja akiwa na maumivu ya tumbo, kutokana na maumivu hayo hakuweza kutembea sawasawa lakini kwa neema ya Mungu wetu aliweza kupokea uponyaji wake na kuwa mzima.

                                  Dada Mary Nyoni akishuhudia matendo makuu ya Mungu.
Akiweza kuinama mara baada ya kupokea uponyaji hii ikionyesha kuwa maumivu yote yamemwacha kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.

3. Fibrana Saliboko alifunguliwa kutoka katika kifungo cha kupooza hakuweza kutembea kwa muda mrefu na alikuwa akitembea kwa kutumia magongo lakini Yesu Kristo wa Nazareth alimponya na alitembea bila ya msaada wa magongo.

 Hapa akiingia kwenye nyumba ya Mungu, Zoe LCM akitembea kwa msaada wa fimbo.

                   Mara baada ya maombi akitembea bila ya msaada wa gongo wala kushikiliwa.
                                          
                                            Akitembea bila ya msaada wa aina yoyote.

                                     Wakupewa utukufu  na heshima ni Yesu Kristo wa Nazareth.