Maelfu wanaofika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe hupata neema ya kusikia neno la kinabii linalotoka kwa Mungu mwenyewe akimtumia mtumishi wake Prophet Joseph, Prophet anapotoa neno la kinabii si neno lake bali ni neno kutoka kwa Mungu mwenyewe kama biblia inavyosema katika kitabu cha
2 Petro 1:20-21 inasema; 20. Awali ya yote,yawapasa mjue kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliofasiriwa kama apendavyo mtu mwenyewe. (21.)Kwa maana unabii haukuja kamwe kwa mapenzi ya wanadamu ,bali watu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Neno la kinabii huleta amani,furaha,suluhisho kufunguliwa na kuwekwa huru.
Kaka yetu alipata neema ya kusikia kutoka kwa Mungu kupitia Prophet Joseph. Kaka yetu alikuwa kila anachofanya hakifanikiwi na amekuwa akiota mtu anamfukuza na pia Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph akiongozwa na Roho aliendelea kumweleza kuwa amekuwa akiota anapanda treni lakini tofauti na ilivyozoeleka amekuwa akiota anapanda treni ya mbele kaka huyu ndipo alipokiri kuwa ni kweli mambo yote hayo ndiyo yanayomtokea kwenye maisha yake.
Ikafika wakati wa kaka huyu kuwekwa huru na Yesu Kristo wa Nazareth.
Akiwekwa huru kutoka katika mateso hayo yote.
2. Mama huyu naye alipata neema hiyo ya kusikia kutoka kwa Mungu kupitia Prophet Joseph, Prophet alimwendea mama huyu na kumweleza kuwa amekuwa akisubuliwa na kifua kuuma na mbavu kubana kwa muda mrefu na hadi kupelekea mama huyu kudhania kuwa anasumbuliwa na Asthma mama huyu akakiri ni kweli kabisa, lakini Prophet Joseph akiongozwa na Roho aliendelea kumweleza mama huyu kuwa si ugonjwa wa Asthma kama mama huyu anavyodhani bali ni uonevu wa shetani, na pia alimweleza mama huyu kuwa anasumbuliwa na presha ya chini mama huyu alimshangaa Mungu sana na kusema ni kweli kabisa anapitia mambo yote hayo.
Akifunguliwa kutoka katika roho chafu za magonjwa.
3. Mama huyu pia alipata neno la kinabii kuwa amekuwa akipatwa na hasira za mara kwa mara jambo dogo tu humfanya apandwe hasira kwa haraka mama huyu akakiri ni kweli kabisa na amejaribu kuacha ameshindwa kabisa ndipo ulipofika wakati wa Yesu Kristo kumweka huru kabisa kutoka katika roho chafu ya hasira.
Akikiri kuwa ni kweli amekuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu.
Prophet Joseph akimfungua kwa jina la Yesu Kristo kutoka katika hali hiyo.
4. Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alimwendea kaka yetu na kumweleza kuwa kaka huyu amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya magoti kwa muda mrefu amekuwa akishindwa kuinama au kuchuchumaa kaka yetu akakiri ni kweli kabisa amekuwa akipata maumivu hayo.
Prophet Joseph akiifukuza roho ya maumivu kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Roho hiyo ya maumivu ikimwacha kaka huyu .
5. Pia mama huyu alipata neema ya kusikia kutoka kwa Mungu, Prophet Joseph alimfwata mama huyu na kumwambia kuwa mama huyu amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo na mabega mara kwa mara mama huyu alikiri kuwa ni sahihi kabisa anayosema mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph.
MAMA HUYU AKIWEKWA HURU KUTOKA KATIKA ROHO HIYO CHAFU YA MAUMIVU
Akiwa amechukuliwa na nguvu ya Mungu.
Prophet Joseph akimfungua mama huyu.
Mungu anaendelea kuzungumza na watu wake kupitia watumishi wake. Utukufu na Sifa ni kwake yeye mwenye uwezo na nguvu zote! Jina la Bwana Libarikiwe!!!