TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 31 August 2014

PROFESSOR JAY AKIMFURAHIA MUNGU WA ZOE

Mwanamziki wa bongo fleva Joseph Haule au kwa jina la kisanii Professor Jay akimshukuru Mungu kwa kumtoa katika roho ya ulevi na pia anamshukuru Mungu sana kwa maana alikuja katika huduma hii ya Life in Christ Ministries Zoe akiwa na maumivu ya miguu lakini Mungu alimponya kabisa na alisema ana kila sababu ya kuendelea kumshukuru Mungu kwasababu amekuwa kwenye sanaa kwa muda usiopungua miaka 20 lakini hakuwa na mafanikio kama aliyonayo sasa baada ya kumpokea Yesu Kristo wa Nazareth.


Hapa Professor Jay akiwa katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe.

Professor Jay akishuhudia maelfu ya waliofika katika huduma ya LCM jinsi ambavyo Mungu amemtendea.





Professor Jay akimwimbia Mungu katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe... Hakika sanaa bila Mungu haiwezekani.Utukufu na sifa kwa Mungu mwenye uwezo wote.

MUNGU NI MWEMA

Hakuna litakalo endelea kwenye nyumba ya  Mungu Life in Christ Ministries Zoe, bila Mungu kumfunulia Prophet wake,wakati ibada ikiendelea kijana huyu alikutwa na Security akizunguka zunguka katika eneo la kuegesha magari,ndipo mmoja wa security alipomleta ndani ya kanisa, Prophet Joseph akamuuliza baba yake wa mbinguni ndipo akapokea ujumbe kutoka kwa baba wa mbinguni kwamba "Muonyeshe kijana huyu kuwa hii ni nyumba yangu" Prophet Joseph akasema kuwa kijana huyu ana roho ya wizi na hapaswi kulaumiwa kwani adui yetu si mtu bali ni shetani.



Mmoja kati ya masecurity wa LCM Zoe akimwingiza kaka huyu ndani ya kanisa.


Prophet Joseph akimuombea kaka huyu roho chafu ya wizi imuachie." Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa". Luka 6:37.


                         Prophet Joseph akiifukuza roho ya wizi kwa kaka huyu.


Akimshukuru Mungu kwa kumweka huru kutoka katika kifungo cha wizi.

Yohana 10:10,Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. 









YOTE YAWEZEKANA KWAKE YEYE AAMINIYE

Ndugu hawa waliweza kupokea uponyaji wao baada ya Prophet Joseph kusoma neno la Mungu kutoka katika kitabu cha Zaburi 107:20, "Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao".  Pindi neno hili liliposomwa watu walipokea uponyaji wao na kufunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali. Hawa  ni baadhi ya maelfu waliofika katika huduma ya LIFE IN CHRIST MINISTRIES ZOE na kupokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth akimtumia mtumishi wake Prophet Joseph.

 Dada Joyce kutokea Mwanza alikuja akiwa na maumivu ya mgongo baada ya kusoma neno hilo alipokea uzima hapo hapo,hapa akimshukuru Mungu kwa kumponya.
Dada Joyce akiwa ameinama kuonyesha kwamba hana tena maumivu ya mgongo.
Dada yetu Amina kutoka Rufiji alikuja akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo na pia alikuwa hawezi kukaa kwenye mkusanyiko wa watu wengi kutokana na ugonjwa huo lakini baada ya kusoma neno hilo la Mungu alipokea uponyaji wake mara moja.

                                Yanayoshindikana kwa wanadamu kwa Mungu yanawezekana .