Leornard Kasanga alifika katika nyumba ya Mungu, Zoe L.C.M akisumbuliwa na kansa ya ini kutokana na kuugua kansa hiyo tumbo lake lilijaa sana, hakuweza kutembea na kula na ilipelekea kuwa dhaifu sana. Alipofika kwenye nyumba ya Mungu hakuweza kukaa ilibidi apumzishwe kwenye sehemu maalum. Prophet Joseph ndipo alipomuita Mungu mponyaji ili aweze kumponya kaka yetu, kwa neema ya Mungu na rehema za Mungu ndugu yetu aliweza kupokea uponyaji wake na papo hapo akasimama na kutembea bila ya kushikiliwa.
Ndugu Leornard akiwa kwenye machela.
Akiwa ameshikilia tumbo lake.
Aliweza kusimama mara baada ya maombi.
Akitembea bila ya msaada wa mtu mwingine.
Akiwa amejitwika machela baada tu ya kupokea uponyaji wake.
Akimtukuza Mungu kwa kumponya.
Akishuhudia yale matendo makuu ya Mungu aliyomtendea.
Akionekana mwenye furaha.
Hakika hii ni kuonyesha kuwa Mungu ni mkuu, aliweza hata kukimbia baada ya kutokuweza kwa muda mrefu.
YESU NI YEYE YULE JANA NA HATA MILELE.
SIFA NA UTUKUFU KWA BWANA.