TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Thursday, 19 March 2015

KIFUNGO CHA POMBE CHA MUDA MREFU CHAMUACHA KWA JINA LA YESU KRISTO

Ndugu Goodluck Mbuya aliwekwa huru kwenye mstari wa uponyaji katika ibada ya jumapili tarehe 15/3/2015, aliwekwa huru kutoka katika roho ya ulevi ambayo ilikuwa ikimtesa kwa miaka mingi alijaribu kuacha kwa akili zake lakini haikuwezekana mpaka alipoamua kuja kupata msaada kutoka kwa Yesu Kristo mponyaji ndipo alipowekwa huru na Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai.


                             Ndugu Goodluck akiwa kwenye mstari wa uponyaji.
                        Prophet Joseph akimuombea kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
                           Roho chafu ya pombe ikifukuzwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
 Baada ya maombi alijaribu pombe na alishindwa kuinywa hii ni kuonyesha hakika Yesu Kristo amemtoa kwenye kifungo cha pombe.
                                                   Akitapika pombe hiyo.
Akitokwa machozi ya furaha, mwana wa Mungu akikuweka huru hakika unakuwa huru kweli kweli.

                                               Utukufu kwa Yesu Kristo wa Nazareth.











BAADA YA OPARESHENI KUSHINDIKANA APATA JIBU LAKE KWA YESU KRISTO WA NAZARETH

Winfrida Mwingira miaka saba iliyopita alipata ajali ya gari iliyosababisha mguu wake ukatwe mara 3 na pia alifanyiwa oparesheni  kubwa 7 na alilazwa katika hospitali ya taifa Muhimbili kwa miaka 3 lakini maumivu hayakumwacha kabisa na alitakiwa aende kwenye oparesheni ya nne lakini alikataa na kuamini kuwa sasa ni wakati wa Bwana kumponya yaliyoshindikana kwa wanadamu kwa Mungu yanawezekana. Kwa miaka saba amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya nyonga na alikuwa hawezi kukaa wala kusimama alikuwa ni mtu wa kulala na kila kitu alikuwa akimalizia kitandani na alikuwa akisaidia na mume wake mpenzi. Aliweza kupokea uponyaji wake kwa kupitia neno la uzima tu lililoongozwa na mtumishi wa Mungu Prophet Joseph lililokuwa na kichwa cha habari " Wajue Wakristo" na kwa neno hilo dada Winfrida alipokea uponyaji wake papo hapo. Kutokana na maumivu ya nyonga hakuweza hata kupiga hatua kumi lakini kwa neema ya Mungu alipopokea uponyaji aliweza kucheza na kutembea mwenyewe bila ya kuwa na maumivu ya aina yoyote.

                                   Akiingia kwenye nyumba ya Mungu LCM Zoe.


Akiwa amesimama na huo mkeka unaonekana pichani ndio aliokuja nao ili autumie kupumzishia mwilini maana akikaa kwa muda mrefu alikuwa anapata maumivu makali sana.
                         Akipita mbele kuja kushuhudia yale ambayo Mungu amemtendea.
 Akiwa ni mwenye furaha mara baada ya kupokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.


                                       Akimchezea Mungu kwa furaha.
                           Akishuhudia matendo makuu ya Mungu katika maisha yake.
                                        Akimshukuru Mungu kwa aliyomtendea.
                                           Akitokwa machozi ya furaha.

Akionekana mwenye furaha sana hakika inatupasa kushukuru kwa kila jambo, dada Winifrida akiwa ameponywa na maumivu yote kumwacha kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.







MATENDO MAKUU YA MUNGU YANAENDELEA KUTUSHANGAZA

Hakika Mungu wetu ameendelea kutushangaza kwa matendo yake makuu anayoyatenda, dada Happy Marko kutoka Mkuranga alifika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe akiwa hajiwezi kabisa kutokana na kupooza mwili hakuweza hata kutingisha mikono wala vidole vyake. Wakati mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alipokuwa akikemea roho zote za kupooza dada Happy alikuwa amebebwa  na wainjilisti akielekea maliwato (chooni) ndipo nguvu kutoka juu ilimshukia na kufukuza roho zote za kupooza na ghafla alisimama mwenyewe kwa miguu yake bila ya kushikiliwa na mtu yoyote. Happy alipokea uponyaji huo kutoka Mbinguni kwa baba bila hata ya kuwekewa mkono lakini aliamini kuwa Yesu Kristo anaponya na yeye atapokea uzima na ndivyo ilivyokuwa kwake.


              Dada Happy akiingia kwenye nyumba ya Mungu huku akiwa amebebwa .
                                           Akiwa ndani ya nyumba ya Mungu.
                  Mara baada ya maombi akiwa amesimama bila ya kushikiliwa wala kubebwa.

           Mmoja kati ya wainjilisti waliokuwa wakimbeba akishuhudia na kumtukuza Mungu.
                              Akishuhudia na kumshukuru Mungu kwa kumponya.
                          Ndugu wa dada Happy wakimshukuru Mungu kwa kumponya ndugu yao.
                              Mtoto wa dada Happy akibubujikwa machozi ya furaha.
 Akinyanyuka mara baada ya ugonjwa wa kupooza kumwacha na kuwa huru kama anavyoonekana.
Akiwa amesimama vizuri maana ugonjwa wa kupooza sio sehemu ya maisha yake na Yesu Kristo akiwa amemuweka huru moja kwa moja.

                                            Utukufu kwa Yesu Kristo.