TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Thursday, 19 March 2015

BAADA YA OPARESHENI KUSHINDIKANA APATA JIBU LAKE KWA YESU KRISTO WA NAZARETH

Winfrida Mwingira miaka saba iliyopita alipata ajali ya gari iliyosababisha mguu wake ukatwe mara 3 na pia alifanyiwa oparesheni  kubwa 7 na alilazwa katika hospitali ya taifa Muhimbili kwa miaka 3 lakini maumivu hayakumwacha kabisa na alitakiwa aende kwenye oparesheni ya nne lakini alikataa na kuamini kuwa sasa ni wakati wa Bwana kumponya yaliyoshindikana kwa wanadamu kwa Mungu yanawezekana. Kwa miaka saba amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya nyonga na alikuwa hawezi kukaa wala kusimama alikuwa ni mtu wa kulala na kila kitu alikuwa akimalizia kitandani na alikuwa akisaidia na mume wake mpenzi. Aliweza kupokea uponyaji wake kwa kupitia neno la uzima tu lililoongozwa na mtumishi wa Mungu Prophet Joseph lililokuwa na kichwa cha habari " Wajue Wakristo" na kwa neno hilo dada Winfrida alipokea uponyaji wake papo hapo. Kutokana na maumivu ya nyonga hakuweza hata kupiga hatua kumi lakini kwa neema ya Mungu alipopokea uponyaji aliweza kucheza na kutembea mwenyewe bila ya kuwa na maumivu ya aina yoyote.

                                   Akiingia kwenye nyumba ya Mungu LCM Zoe.


Akiwa amesimama na huo mkeka unaonekana pichani ndio aliokuja nao ili autumie kupumzishia mwilini maana akikaa kwa muda mrefu alikuwa anapata maumivu makali sana.
                         Akipita mbele kuja kushuhudia yale ambayo Mungu amemtendea.
 Akiwa ni mwenye furaha mara baada ya kupokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.


                                       Akimchezea Mungu kwa furaha.
                           Akishuhudia matendo makuu ya Mungu katika maisha yake.
                                        Akimshukuru Mungu kwa aliyomtendea.
                                           Akitokwa machozi ya furaha.

Akionekana mwenye furaha sana hakika inatupasa kushukuru kwa kila jambo, dada Winifrida akiwa ameponywa na maumivu yote kumwacha kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.







No comments:

Post a Comment