TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 1 March 2015

MAUMIVU MAKALI YA MWILI YAMWACHA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Philipo Lucas kutoka Simanjiro, Arusha alipta ajali ya gari mnamo mwaka 2010 na kusababisha maumivu mwili mzima na hakuweza kutemea sawasaw ndipo kwa neema y aMungu aliweza kukutana na rafiki yake, rafiki yake akampa gazeti la Nyakati ambalo katika ukurasa wa 2 wa gazeti la Nyakati kuna shuhuda kutoka LCM Zoe za watu walioungwa mifupa na Yesu Kristo wa Nazareth. Mara baada ya kusoma na kuona jinsi Mungu anavyomtumia mtumishi wake Prophet Joseph ndugu Philipo aliamua kufika katika huduma hii, hakika Mungu hakumwacha alipofika alipokea uponyaji wake mara moja na maumivu yote yakamwacha.

                                  Ndugu Philipo akienda mbele kushuhudia.
                                       Akiwa mbele ya madhabahu tayari kushuhudia.
                                             Akishuhudia jinsi Mungu alivyomponya.



MFUPA ULIOPISHANA WANYOOKA NA KUUNGA KWA JINA LA YESU KRISTO.


Obute Obunya alifika katika huduma ya LCM Zoe akiwa na maumivu katika mkono wake wa kushoto kutokana na mkono wake kuvunjika na kusababisha mifupa kupishana, alifika akiwa na hogo mkononi mwake. Wakati mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph alipokuwa akikemea kila roho za maumivu kuwaacha watu ndugu Obute alipokea uponyaji wake, kutokana na maumivu hayo hakuweza kuendesha gari lake, kupiga makofi wala kunyosha mkono huo juu, kwa neema ya Mungu alipopokea uponyaji wake aliweza kuendesha gari yake na kunyosha mkono wake juu. Afisa muuguzi kutoka katika hospitali ya Taifa ya Temeke alithibitisha kwa kusoma X- ray ya ndugu Obute na kuonyesha kuwa mfupa ulikuwa umepishana na kwa neema ya Mungu mfupa uliunga mara moja.

                          Ndugu Obute akiingia kwenye nyumba ya Mungu, LCM Zoe.
                                         Mkono unavyoonekana ukiwa na hogo.

                                Mara baada ya maombi aliweza kuunyosha mkono wake.
                                  Akishuhudia matendo makuu ya Mungu aliyomtendea.
                       Aliweza kupiga makofi kwa mara ya kwanza mara baada ya kupokea uponyaji.
                                                 Afisa muuguzi akikagua mkono huo.
                  Kamba iliyokuwa imeshikilia hogo ikiwa chini mara tu baada ya mfupa kuunga.
                     Mke wa ndugu Obute akimshukuru Mungu kwa kumponya mumewe.
                                                   X- ray ya ndugu Obute.
                Akiendesha gari ambalo mwanzo hakuweza kutokana na maumivu aliyokuwa nayo.
               Akiingia huku akiendesha gari kuonyesha kuwa hakika Mungu ameunga mfupa wake.