TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Monday, 25 May 2015

MIFUPA YA MGUU YAUNGA KWA JINA LA YESU KRISTO

Ndugu Shemkiwa Sheiza alivunjika mfupa wa mguu wake wa kushoto na kusababisha ashindwe kutembea sawasawa alifika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe  akiwa na maumivu kwenye mguu wake uliokuwa umefungwa POP kwa neema ya Mungu wakati wa mstari wa uponyaji alipokea uponyaji wake.

                                           Akiingia kwenye nyumba ya Mungu.
                           Prophet Joseph akimwombea kwa ina la Yesu Kristo.

                                                Akitembea bila ya maumivu yoyote.
                                           Akishuhudia na kusema hasikii tena maumivu.
                          Akitoa hogo mguuni kwake mara baada ya kupokea uponyaji.
Akiwa ni mwenye furaha mara baada ya kupokea uponyaji na kuondoa hogo.

                               UTUKUFU KWA YESU KRISTO WA NAZARETH.

KANSA YA KOO YAFIKIA MWISHO BAADA YA KUKUTANA NA NGUVU YA UFUFUO

Adolf Mutawe alifika katika nyumba ya Mungu, Life in Christ Ministries Zoe, akiwa dhaifu sana kutokana na kusumbuliwa na kansa ya koo. Kutokana na kansa hiyo ya koo haikuwa rahisi kwa ndugu Adolf kumeza chakula na hata kunywa maji ndipo ilipobidi madaktari wamwekee mpira kwenye koo ili aweze kula.
Kansa hiyo ilienea kwenye kifua, mapafu na hadi kufikia mgongoni pia kutokana na kansa hiyo alikuwa akikosa haja kubwa hata kwa wiki mbili mfululizo. Haikuishia hapo ilikuwa ngumu sana kwake hata kumeza mate kutokana nakansa hiyo kuwa kwenye koo ilimlazimu kutema mate kila mara, na pia alikuwa hana nguvu kabisa mwilini mwake.
Mtumishi wa Mungu prophet Joseph akiongozwa na Roho Mtakatifu aliwaelekeza watenda kazi kumbeba ndugu Adolf kwenye kitanda maalum na kumleta hadi madhabahuni ili ndugu Adolf apokee uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth. Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alimwekea mkono kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth kansa ikafukuzwa kutoka katika mwili wa ndugu Adolf na kwa nguvu ya ufufuo kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo alipokea nguvu na uzima ukaingia ndani yake na kansa ikamwacha kwa jina lipitalo majina yote, jina la Yesu Kristo.

       Ndugu Adolf akiwa maejipumzisha kwenye mkeka ndani ya nyumba ya Mungu. LCM Zoe.
                               Prophet Joseph akimtizama ndugu Adolf.
                  Watenda kazi wa LCM Zoe wakimweka kwenye kitanda maalum.
                                 Wakimbeba ili kumpeleka madhabahuni.
                Wakimweka ndugu Adolf madhabahuni tayari kwa kupokea uponyaji wake.
                             Mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph akimuhudumia.
                        Prophet Joseph akiondoa kila udhaifu kwa jina la Yesu Kristo.
             Prophet Joseph akimsaidia kutoka katika kitanda hicho mara baada ya maombi.

                                              Akitembea mwenyewe bila kubebwa.
                            Ndugu Adolf akimshukuru Mungu kwa kumponya.
 Watenda kazi wakirudisha kitanda maana ndugu Adolf ameshapokea uzima haihitaji kubebwa tena.
              Mkeka ukiwa umekunjwa kuonyesha kuwa hakika ndugu Adolf amepokea uzima.
                     Akinywa maji bila ya matatizo yoyote mara baada ya kupokea uzima.

                                Hakika hii inaonyesha kuwa ni kweli ndugu Adolf kapokea nguvu mpya.
                                                  Akicheza kwa furaha kwa utukufu wa Mungu.

                                                                  Akilia machozi ya furaha.

Je! ni jambo gani Mungu asiloweza??? Hakuna cha kumshinda Mungu haijalishi tatizo ulilonalo. Ukiamini tu utapokea haja ya moyo wako kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.