TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 12 October 2014

UPONYAJI WAKATI WA MASS DELIVERANCE.

Mungu wetu bado anaendelea kuonekana kwenye maisha ya watu wake, tumemuona akiwagusa, kuwaponya na kuwafungua watu wake.Jumapili aliwaponya na kuwagusa maelfu waliofika katika huduma hii ya LIFE IN CHRIST MINISTRIES ZOE, Hakika ukifika mahali hapa hutarudi kama ulivyokuja.Amini tu.

Dada Hafsa Kazinje alikuja akiwa na maumivu ya mwili lakini wakati wa Mass deliverance alipokea uponyaji wake na kuwa mazima kwa jina la Yesu Kristo.

                                                Akimshuhudia Mungu kwa kumponya.


Dada Devotha Kilave kutoka Morogoro alikuja akiwa na maumivu ya mwili hakuweza hata kulala wala kugeuka,baada ya maombi alipokea uponyaji wake kwa jina la Yesu Kristo.
                                    Hapa akielezea jinsi ambavyo amepokea uponyaji wake.


                      Baada ya maombi aliweza kulala na kugeuka bila ya kuwa na maumivu yoyote.
                                             Hapa akiinama bila ya kuwa na maumivu.
                               Akigeuka ishara ya kuwa maumivu sio sehemu yake tena.
                                                     Akimshukuru Mungu kwa kumponya.

APOKEA UPONYAJI BAADA YA KUUNGUA MOTO.

Adina Kipaya alipata ajali ya kuunga na maji ya moto katika sehemu ya mkono na makalio, walifika katika huduma siku ya tukio,siku ya alhamisi akiwa ni mwenye maumivu makali lakini mtumishi wa Mungu,Prophet Joseph alipomuombea maumivu yalimwacha palepale na aliweza kupata usingizi hapohapo. Alipofika Hospitalini madaktari walishangaa sana maana hakuwa na maumivu ya aina yoyote.

Alikuja katika ibada ya jumapili na mama yake na Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alimwombea na kuwa mzima kabisa na aliweza kuunyanyua juu mkono wake hata yeye mwenyewe aliweza kumshangaa Mungu sana kwa uponyaji huo.Adina na mama yake walimtukuza Mungu sana na kuishia kububujikwa na machozi ya furaha. Na Prophet Joseph alimwambia kuwa kila baada ya dakika tatu pale ngozi ilipotoka itakuja ngozi mpya.Hakika Mungu bado anaendelea kutushangaza.

                             Mwinjilisti Joseph akiwahoji Adina na mama yake.
                                     Jinsi ambavyo mkono wa Adina ulivyokuwa.



                                                         Adina na mama yake .
                  Akiweza kukunja ngumi baada ya mtumishi wa Mungu,Prophet Joseph kumuombea.





                                         Akimshukuru Mungu kwa kumponya mkono.
                        Akibubujikwa na machozi ya furaha baada ya kupokea uponyaji huo.




Hakika iliwapasa kumshukuru Mungu kwa maana hakuna awezaye kuyatenda matendo makuu namna hii isipokuwa Baba yetu wa Mbinguni akimtumia prophet Joseph.
Tunamshukuru Mungu kwa uponyaji huu wa dada Adina Kipaya.

Yeremia 30:17a-" Lakini nitakurudishia afya yako na kuyaponya majeraha yako asema Bwana".







UPONYAJI WAKATI WA MASS DELIVERANCE

Agness Patrick kutoka Morogoro alikuja akiwa amevunjika mkono wake wa kushoto lakini jinsi Mungu wetu alivyomwaminifu mara baada ya Mass deliverance aliweza kupokea uponyaji wake mara moja, alikuja akiwa na POP mkononi lakini baada ya kupokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo nesi kutoka kitengo cha mifupa M.O.I aliweza kumtoa mama huyu POP na akaweza kuunyosha mkono huo bila ya maumivu yoyote.


            Mama Agness akiwa anaingia hapa Life in Christ Ministries Zoe,katika eneo la mapokezi.
                                     Mwinjilisti Joyce akimuhoji mama Agness.
                                  Hapa tunaona mama huyu akichukuliwa na nguvu ya Mungu.
Akiwa chini baada ya nguvu ya Mungu kumchukua,nguvu ambayo hufungua,huvunja kila aina ya nira.

                       Akitoa ushuhuda baada ya kupokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.
         Baada ya maombi aliweza kuunyosha mkono wake,kabla ya maombi hakuweza kuunyosha.
 Nesi kutoka kitengo cha mifupa,MOI, Mrs.Sophia Wellya akithibitisha kuwa ni kweli mfupa umeunga.
                             Nesi akimchukua mama huyu ili akakate hogo.
                 Hogo likiwa limeondolewa ishara ya kwamba mama huyu haihitaji tena hogo hili.
          Hogo likiwa limetupwa chini halihitajiki tena katika mkono wa mama huyu kwa jina la Yesu Kristo.


Mama huyu akilitundika hogo hili kwenye ukuta wa uponyaji hii ikimaanisha kuwa yeye ni mzima na hatalivaa tena hogo hili. Yesu Kristo wa Nazareth anaunga mifupa hata sasa.

















UDHIHIRISHO WA NGUVU YA MUNGU

Muda wa kumwabudu Mungu ulipofika kwakweli tulishuhudia nguvu za Mungu zikiwagusa watu kwa aina ya tofauti kabisa, watu walifunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali. Hakika ukiamini tu Mungu hawezi kukuacha unachotakiwa ni kuamini kwamba Mungu anaweza kukufungua kutoka katika kila aina ya kifungo ambacho adui amekuunganisha nacho. Amini kwamba Mungu hawezi kukuacha kamwe.



                     Baadhi ya watu wakiwa chini baada ya nguvu ya Mungu kuwashukia.



                 Mtumishi wa Mungu,Prophet Joseph akimfungua dada huyu kwa jina la Yesu Kristo.



                             Dada huyu akitapika kila aina ya sumu iliyokuwa mwilini mwake.
                     Prophet Joseph akimfungua kaka huyu kutoka katika kila aina ya uonevu wa ibilisi.

                         Kila nira lazima ivunjwe kwa jina la YESU KRISTO wa NAZARETH.