TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 12 October 2014

APOKEA UPONYAJI BAADA YA KUUNGUA MOTO.

Adina Kipaya alipata ajali ya kuunga na maji ya moto katika sehemu ya mkono na makalio, walifika katika huduma siku ya tukio,siku ya alhamisi akiwa ni mwenye maumivu makali lakini mtumishi wa Mungu,Prophet Joseph alipomuombea maumivu yalimwacha palepale na aliweza kupata usingizi hapohapo. Alipofika Hospitalini madaktari walishangaa sana maana hakuwa na maumivu ya aina yoyote.

Alikuja katika ibada ya jumapili na mama yake na Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alimwombea na kuwa mzima kabisa na aliweza kuunyanyua juu mkono wake hata yeye mwenyewe aliweza kumshangaa Mungu sana kwa uponyaji huo.Adina na mama yake walimtukuza Mungu sana na kuishia kububujikwa na machozi ya furaha. Na Prophet Joseph alimwambia kuwa kila baada ya dakika tatu pale ngozi ilipotoka itakuja ngozi mpya.Hakika Mungu bado anaendelea kutushangaza.

                             Mwinjilisti Joseph akiwahoji Adina na mama yake.
                                     Jinsi ambavyo mkono wa Adina ulivyokuwa.



                                                         Adina na mama yake .
                  Akiweza kukunja ngumi baada ya mtumishi wa Mungu,Prophet Joseph kumuombea.





                                         Akimshukuru Mungu kwa kumponya mkono.
                        Akibubujikwa na machozi ya furaha baada ya kupokea uponyaji huo.




Hakika iliwapasa kumshukuru Mungu kwa maana hakuna awezaye kuyatenda matendo makuu namna hii isipokuwa Baba yetu wa Mbinguni akimtumia prophet Joseph.
Tunamshukuru Mungu kwa uponyaji huu wa dada Adina Kipaya.

Yeremia 30:17a-" Lakini nitakurudishia afya yako na kuyaponya majeraha yako asema Bwana".







No comments:

Post a Comment