TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Thursday, 26 March 2015

RIBA YA BENKI YATEREMSHWA KWA MAOMBI


Hakika Mungu anaweza kutenda zaidi ya tunavyoomba kaka Innocent Chonya alifika katika mstari wa uponyaji na kuonyesha shauku kutokana na kwamba alikuwa maechukua mkopo katika mojawapo ya benki hapa nchini Tanzania lakini riba yake ilikuwa ni 19% na alikuwa maeandika barua kwenye benki hiyo akiwaomba kuteremsha hadi kwa asilimia 17 alipofika kwa mtumishi wa Mungu prophet Joseph  akamwombea na majibu aliyoyapata kutoka kwenye benki hiyo ni ya kushangaza sana maana walipunguza zaidi ya alivyoomba walipunguza hadi kwa asilimia 16, Mungu wetu anashangaza sana. Alipofika kutoa ushuhuda prophet Joseph alimpa neno la kinabii kuwa sio kwamba wamepunguza bali watalifuta deni lenyewe kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.

 Hii ikiwa ni barua aliyokuwa amekuja nayo kwenye mstari wa uponyaji jumapili ya tarehe 15/3/2015
                     Mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph akimwombea kwa jina la Yesu Kristo.
                                      Jumapili ya tarehe 22/3/2015 alipofika kushuhudia.
                                          Akimshukuru Mungu kwa kumtendea.


                                     Nguvu ya Mungu ikiwa imemchukua.

                              UTUKUFU KWA MUNGU MWENYE NGUVU NA UWEZO.



AWEKWA HURU KUTOKA KATIKA MTEGO WA IBILISI


Janeth Mkwawa alipata ajali jumatatu iliyopita, aliteleza akiwa nyumbani kwake na kutegua mguu wake na kusababisha sehemu ya mfupa kuwa nje kutokana na mguu huo kupasuka. Alikwenda hopsitalini na kushonwa nyuzi saba alifika katika nyumba ya Mungu Zoe akiwa hajiwezi alikuwa akitembea kwa shida na maumivu makali, alipokea uponyaji baada ya mtumishi wa Mungu Prophet Joseph kuamuru roho chafu za magonjwa kuwaacha watu kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth. Ndipo alifika mbele kutoa ushuhuda mtumishi wa Mungu Prophet Joseph akasema dada Janet anahitaji kuwekwa huru tena kwasababu anachikiona ni kuwa mpango wa ibilisi ni kusababisha dada Janeth arudi hospitali tena na takaporudi kufanyiwa operasheni ibilisi atamtega na kusababisha madaktari kumkata mguu huo, wakati akiamuru kila roho chafu kumwacha dada huyu roho chafu zikakiri kuwa ni kweli ndio mpango wao ambao wameupanga kwa dada huyu lakini kwakuwa hakuna nguvu inayoweza kushindana na nguvu ya Mungu dada huyu aliwekwa huru kutoka katika mtego huo wa ibilisi.

                                            Akishuhudia jinsi Mungu alivyomponya.
                                                          Mguu huo ulivyokuwa.

                                             Akitembea bila ya kuwa na maumivu yoyote.

             Akimshangilia Mungu kwa kumweka huru kutoka katika mitego ya ibilisi.

                             Mwana wa Mungu akikuweka huru unakuwa huru kweli kweli.

MFUPA WAUNGA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Festia Ijegere alipatwa na hali isiyokuwa ya kawaida akiwa navuka barabara , akiwa katikati ya barabara mshipa katika mguu wake ulipasuka na alishindwa kutembea sawasawa kutokea siku hiyo hakuweza kutembea wala kubeba vitu vizito. Wakati wa maombi aliweza kupokea uponyaji wake na kuweza kutembea sawasawa.


                                       Akiwa mbele kushuhudia jinsi Mungu alivyomponya.
                                                 Mguu huo unavyoonekana.
 Aliweza kukunja goti lake mara baada ya kupokea uzima kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.
                                          Hapa akiunyosha bila ya kuwa na maumivu yoyote.
 Hivi ndivyo mguu wake unavyoonekana kwenye X ray aliyokuja nayo kwenye nyumba ya Mungu LCM Zoe.

                                    Mungu anatenda hata sasa ukiamini.




AACHA KUTEMBELEA WHEEL CHAIR KWA NENO LA UZIMA


Glory Elijah hakika alikuwa na kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu ambayo amemfanyia kwenye maisha yake. Dada Glory alifika kwenye nyumba ya Mungu akiwa anatumia kiti maalum cha walemavu yaani wheel chair kutokana na kuanguka na kusababisha mvunjiko na kusababisha mfupa kupishana hakuweza kutembea  mwenyewe na alitakiwa kwenda kwenye oparesheni. Baada ya mtumishi wa Mungu Prophet Joseph kufundisha neno la Mungu lenye uzima  na kuamuru uponyaji kwa kila mwenye ugonjwa dada yetu alipokea uponyaji na akaweza kutembea bila ya kutumia kiti hicho.

                     Dada Glory akiwa kwenye gari lililomleta kwenye nyumba ya Mungu.
                                           Akiwa kwenye wheel chair hiyo.

                                        Akiwa kwenye nyumba ya Mungu LCM ZOE.
                               Mguu huo ukiwa juu ya kiti hakuwa akiweza kuuweka chini.
                  Mara baada ya maombi aliweza kusimama na kutembea mwenyewe.
                      Wheel chair ikiwa juu kuonyesha kuwa hakika Mungu amemponya.

                                                  Akishuhudia  matendo makuu ya Mungu.

                      Hizi ni X ray zikionyesha jinsi ambavyo mfupa ulikuwa umepishana.

                                                          UTUKUFU KWA MUNGU.