Ndugu Laurian Swai alikuwa kwenye kifungo cha utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe. Amekuwa kwenye kifungo hicho kwa muda mrefu, alijaribu kwa akili zake kuacha lakini haikuwezekana. Ndipo alipofika katika nyumba ya Mungu LCM Zoe ili awekwe huru na bwana wetu Yesu Kristo, na hakika Yesu Kristo hakumwacha. Alifika katika mstari wa maombezi na mara alipowekewa mkono na mtumishi wa Mungu prophet Joseph, roho chafu ya pombe na utumiaji wa madawa ya kulevya ilimwacha na ndugu Laurian akawa huru kabisa.
Ndugu Laurian akiwa kwenye mstari wa uponyaji.
Mtumishi wa Mungu prophet Joseph akimhoji ndugu Laurian.
Mtumishi wa Mungu akiifukuza roho chafu za ulevi.
Akiionja pombe aina ya kiroba mara baada ya maombi.
Akitema chini pombe hiyo maana alishindwa kumeza.
Pombe na sigara vikiwa chini mara baada ya ndugu Laurian kufunguliwa kutoka katika kifungo cha ulevi na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Hakika hakuna kifungo ambacho Mungu hawezi kukufungua amini tu nawe utafunguliwa.
SIFA NA UTUKUFU KWA BWANA.