TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 3 May 2015

MFUPA WAUNGA NA NYONGA YAPONA KWA JINA LA YESU KRISTO

Abdul Ramadhan alipata ajali ya pikipiki, kutokana na ajali hiyo mfupa wa mkono na mguu ulivunjika pia nyonga yake iliumia na kumsababishia kutembelea magongo. Alikwenda hospitalini na ilimbidi atoe shilingi millioni 9 za kitanzania kwa ajili ya oparesheni lakini kwa jinsi Mungu alivyo mwema katika maisha ya ndugu yetu, ndugu yetu aliweza kukutana na mtu aliyemweleza neema iliyoko katika nyumba ya Mungu LCM Zoe, na jinsi ambavyo Mungu anamtumia mtumishi wake Prophet Joseph kuwaponya watu wenye matatizo mbalimbali kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth. Ndipo ndugu Abdul alipoamua moyoni mwake kuwa ni lazima afike ili aweze kupata uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo. Hakika kwa imani aliyokuwa nayo alipofika katika nyumba ya Mungu LCM Zoe alipokea uponyaji wake hapo hapo.

                       Ndugu Abdul Ramadhan akiingia kwenye nyumba ya Mungu LCM Zoe.

                  Prophet Joseph akimwombea ndugu Abdul kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.

                                  Akiamuru maumivu ya Nyonga kumwacha ndugu Abdul.
                                  Akiwa amesimama bila ya msaada wa magongo.

                                                    Akitembea bila ya msaada magongo.
                                            Magongo yakiwa chini kwa utukufu wa Mungu.

                  Hakuna tena oparesheni kwa ndugu Abdul, hakika Mungu wetu ni muweza.

                                           UTUKUFU KWA MUNGU BABA.

No comments:

Post a Comment