TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Saturday, 23 May 2015

APOKEA UPONYAJI WA PUMU NA UVIMBE WADONDOKA BILA YA OPARESHENI BALI KWA JINA LA YESU KRISTO


Neema Eliyah kutoka Kimara alifika kwenye nyumba ya Mungu LCM Zoe, kuja kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyomtendea. Alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa pumu kwa muda mrefu na kila mara alipokuwa akipata ujauzito pumu ilikuwa ikimshika zaidi na mara zote alikuwa na tatizo la ujauzito kutoka lakini hakujua kuwa alikuwa na uvimbe "Fibroid" kwenye tumbo lake. Alifika kwenye mstari wa uponyaji ili aombewe pumu imwache, Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alimwombea na mara alipofika nyumbani cha kushangaza tumbo likaanza kumuuma akamwamsha mume wake na kumweleza, ghafla akanza kukohoa na ndipo alipokohoa tu kukatoka mapande makubwa kama ya damu yapatayo kama kilo 5 katika sehemu zake za siri na kudondoka chini, ndio ukawa mwisho wa uvimbe, katika hali ya kawaida ilibidi afanyiwe upasuwaji ili kuondoa uvimbe huo lakini kwa nguvu na neema ya Mungu uvimbe ulitoka bila ya upasuaji. Na ndio ukawa mwisho wa pumu na uvimbe. Utukufu kwa Mungu.

                                             Akiwa kwenye mstari wa uponyaji.
                            Akionyesha jinsi alivyokuwa akitumia dawa za pumu.
                        Mtumishi wa Mungu akifukuza roho ya pumu ndani ya dada Neema.

                                                  JUMAPILI ILIYOFUATIA.
 Akiwa ameshika picha ya uvimbe uliondondoka kutoka kwenye sehemu zake za siri.
                          Akiwa na mume wake wakishuhudia matendo makuu ya Mungu.

                                                                   Uvimbe huo katika picha.


KWA NGUVU YA UFUFUO KANSA YA KONGOSHO YASALIMU AMRI

Nelson Kamwela aliletwa  na mke wake kwenye nyumba ya Mungu Life in Christ  Ministries, Zoe wakitafuta msaada kutoka kwa Mungu mara baada ya madaktari kushindwa. Aliletwa akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya kongosho kwa zaidi ya miezi 6 na kansa hiyo ilienea mwili mzima na kumsababishia maumivu makali sana katika mwili wake.
Haikuwa rahisi kwake kumeza chakula hivyo iliwabidi madaktari kumpasua utumbo mwembamba na kupitisha mpira ili kumsaidia kula kwa kutumia mpira, pia hakuweza kula vyakula vigumu alikuwa akitumia vyakula kama mtori, uji au maziwa ilibidi apitishiwe kwenye mpira kwasababu kila alipokuwa akila alikitapika chakula chote na kusababisha mwili kukosa nguvu.
Alikuwa akitumia matibabu maalum ya kansa ambayo huitwa chemotherapy lakini baada ya muda madaktari hawakuendelea tena na tiba hiyo kutokana na mwili wa ndugu Nelson kuzidi kudhoofika, madaktari wakashauri arudishwe nyumbani mpaka mwili wake utakapopata nguvu ndio arudi kuendelea na matibabu hayo. Kwa neema na upendo wa Mungu walifika mara baada ya kuona hakika hakuna tegemeo lingine isipokuwa kurudi kwa Mungu Baba ambaye ndiye mwenye spare zote za miili yetu na ndiye mponyaji mkuu. Walipofika kwenye ibada mtumishi wa Mungu prophet Joseph akiongozwa na Roho Mtakatifu aliwaomba watenda kazi wa huduma wambebe ndugu Nelson hadi kwenye madhabahu ili aweze kumuombea, hakika Mungu wetu ni mkuu sana ndipo sasa ikawa wakati wa Bwana wetu Yesu Kristo kujidhihirisha ndani ya Mtumishi wake, prophet Joseph alimwombea na mara ndugu Nelson akapokea nguvu ya ufufuo , akasimama na kutembea bila hata ya kushikiliwa hakika kuna nguvu katika jina la Yesu. Hakuwa kutembea kwa muda wote huo aliokuwa mgonjwa na pia ilikuwa ngumu kwake kunywa maji lakini mara baada ya maombi alikunywa maji kwa kutumia kinywa na wala sio mpira tena, pia hakuwa akilala kutokana na maumivu makali alikuwa hadi achomwe sindano ndio alale lakini baada ya maombi hali ya usingizi mzito ilimpata. Ugonjwa wa kansa ya kongosho umesalimu amri kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.

                             Ndugu Nelson akiwa amejilaza kwenye gari iliyomleta.
                                         Akiingizwa kwenye nyumba ya Mungu.

                         Mara baada ya kuingizwa ndani, akiwa amejilaza kwenye mkeka.
               Mpira uliokuwa kwenye tumbo lake, uliokuwa ukitumika kwa kupitishia chakula.

                Watenda kazi wa huduma wakiwa wamembeba kumpeleka madhabahuni.
                                      Akiwa kwenye eneo la madhabahuni .
                    Prophet Joseph akimwombea kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.

                                                   Prophet akimwinua ndugu Nelson.

                                   Akitembea mara baada ya kupokea nguvu kutoka kwa Yesu Kristo.

                                                Akionekana ni mwenye uzima tele.

 Mara baada ya maombi akiwa amekaa kwenye kiti, kitu ambacho hakuweza kwa muda mrefu.
                                     Akinywa maji mara baada ya kupokea uzima.

                Mke wake akimshukuru Mungu kwa kumtendea mambo makubwa kiasi hiki.

                                    HAKUNA JAMBO GUMU LA KUMSHINDA MUNGU.