Matendo 28:8 inasema; Ikawa babake Publio alikuwa hawezi homa na kuhara damu. Paulo akaingia kwake, akaomba,akaweka mikono juu yake, na kumponya. Hata sasa tunashuhudia Mungu akimtumia Mtumishi wake Prophet Joseph kuweka mikono juu ya watu nao kupokea uzima kutoka kwa Yesu Kristo mwenyewe.
Tunaona maelfu ya watu waliofika katika mstari huu wa uponyaji wakipokea uzima na kufunguliwa katika kila mateso ya ibilisi.
Prophet Joseph akimuombea mama huyu ambaye alikuwa akitembelea fimbo.
Mama huyu akifurahia baada ya kupokea uzima kutoka kwa Yesu Kristo.
Roho chafu ikifukuzwa ndani ya mama huyu kwa jina lipitalo majina yote,Jina la Yesu Kristo.
Sunday, 5 October 2014
PRAYERLINE YA WATOTO
Biblia inasema waacheni watoto wadogo waje kwangu wala msiwazuie kwa maana Ufalme wa Mungu ni wao... Mathayo 19:14. Ndivyo tunavyoona watoto wakiwa katika mstari wa uponyaji.
Prophet Joseph akiwagusa watoto hao kama tunavyoona.
Wazazi wakiwa na watoto wao katika prayerline ya watoto.
Prophet Joseph akiwaombea watoto hao waliofika katika Prayerline.
Prophet Joseph akiwagusa watoto hao kama tunavyoona.
Wazazi wakiwa na watoto wao katika prayerline ya watoto.
Prophet Joseph akiwaombea watoto hao waliofika katika Prayerline.
SHUHUDA ZA MAELFU WALIOFUNGULIWA KUTOKA KATIKA VIFUNGO VYA AINA MBALIMBALI
Kwa kila jambo ambalo Mungu anatufanyia yatupasa kushuhudia na kumshukuru kwa kila jambo, ndivyo ilivyokuwa ibada ya jumapili hii katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe, kati ya maelfu waliofunguliwa kutoka katika vifungo vya Ushoga,Usagaji,Umaskini,Kupiga punyeto,kutokufanikiwa na kila aina ya kifungo walifika mahali hapa kushuhudia ukuu wa Mungu na jinsi Mungu alivyobadilisha maisha yao.
Hakika mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi za ibilisi 1Yohana 3:8b.
Baadhi ya maelfu waliofunguliwa kutoka katika kila uonevu wa ibilisi, wakishuhudia jinsi walivyofunguliwa na kuwa hutu kabisa.

SHUHUDA ZA KUFUNGULIWA KUTOKA KATIKA ULEVI WA AINA MBALIMBALI
Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph aliwaita mbele watu wote ambao walifika katika huduma ya Life in Christ Ministries wakiwa katika vifungo vya ulevi,uvutaji bangi,utumiaji wa madawa ya kulevya na kila aina ya ulevi na kufunguliwa na Yesu Kristo ili washuhudie jinsi Mungu alivyowatendea na kuwabadilisha kabisa.
Hawa ni baadhi tu ya kati ya maelfu ya waliofunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali vya ulevi. Hakuna awezaye kumtoa mtu kwenye vifungo isipokuwa Yesu Kristo yeye mwenyewe.
Utukufu na Heshima ni wa kwake Yesu Kristo mtenda miujiza.
Utukufu na Heshima ni wa kwake Yesu Kristo mtenda miujiza.
TUMBO LILILOKUWA WAZI LAPONYWA KWA JINA LA YESU KRISTO
Mungu anaendelea kushangaza kwa ukuu wake dada Lisa John alikuja mwezi wa sita mwaka huu , tatizo lililomfanya afike katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe ni tatizo la tumbo kufumuka, Alilazwa katika hospital ya Amana jijini Dar es salaam ambako alikwenda kujifungua, alijifungua kwa oparesheni lakini kidonda hakikuweza kupona kila mara aliposhonwa tumbo lilifumuka. Ndipo alipoamua kumtafuta daktari wa madaktari Yesu Kristo wa Nazareth kwasababu yeye anaponya madaktari wanatibu. Hakika Mungu alionekana katika maisha ya dada yetu alifika na kuingia katika mstari wa uponyaji ( PRAYER LINE) ambayo hufanyika kila siku ya jumapili ikiongozwa na Roho Mtakatifu mwenyewe kwa kumtumia Mtumishi wake Prophet Joseph,mara mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alipomwekea mkono naye alipokea uzima kidonda kilifunga.
Hii ni picha inayoonyesha tumbo likiwa wazi na utumbo kuonekana.
Dada Lisa akishuhudia matendo makuu ya Mungu aliyomtendea.Hapa akiwa ni mzima kabisa.
Prophet Joseph akimuombea kwa jina la Yesu Kristo uponyaji uendelee kudumu.
Nguvu ya Mungu ikimshukia dada Lisa.
Uponyaji na uzima wapatikana kwa Yesu Kristo. Isaya 53:5,Hakika kwa kupigwa kwake Yesu sisi tumepona Ahsante Yesu Kristo kwa uponyaji na uzima.

HAKUNA JAMBO GUMU LA KUMSHINDA BWANA
Ndugu Francis Mkumbo kutoka Ubungo alivunjika mguu wake mara tatu kutoka na ajali,ilimbidi atumie magongo ndio aweze kutembea alikuja akiwa anatembelea magongo lakini hakuna jambo la kumshinda Yesu Kristo kama katika kitabu cha Mwanzo 18:14 inasema ,Kuna Neno gani gumu la kumshinda Bwana? Hakika hakuna jambo gumu la kumshinda Bwana, Mara baada ya Mass Deliverance ndugu yetu Francis Mkumbo akapata nguvu katika mguu wake na akaweza kutembea bila ya kutumia msaada wa magongo...
Kama tunavyoona katika picha hizi.
Ndugu Francis anaonekana akiwa anatembea bila y amsaada wa magongo.
Hapa akishuhudia baada ya kupokea uponyaji.
Mke wa ndugu Francis akimshukuru Mungu kwa uponyaji.
Hakika Yesu Kristo anaendelea kuponya hata sasa haijalishi ugonjwa,tatizo ulilonalo ukiamini tu kwamba Uzima wapatikana kwake hakika atakuponya.
Pia ndugu yetu Yohana Meshack alikuja akiwa na maumivu ya miguu na kiuno kwa wiki mbili naye alikuja akiwa anatembelea magongo lakini alipokea uponyaji wake na kuwa mzima kabisa.
Akitembea bila ya kutumia gongo.
Akishuhudia kwa kuponywa na Bwana wetu Yesu Kristo.
Hili ndilo gongo alilokuwa anatumia kutembelea akiwa amelitupa kuonyesha kuwa ni kweli amepona.
Mtenda kazi wa Life in Christ Ministries Zoe akilitundika gongo hilo katika ukuta wa uponyaji ikiwa ni ishara kuwa ndugu yetu ni mzima na haihitaji tena kutembelea gongo hilo.
Sifa kwa Bwana wetu Yesu Kristo.!!!

TUNAENDELEA KUMSHUHUDIA YESU KRISTO AKIFUNGUA WATU KUTOKA KWENYE VIFUNGO MBALIMBALI.
Hakika Bwana wetu Yesu Kristo ananendelea kutenda miujiza mpaka sasa, Dada Julieth John alifika katika ibada ya Jumapili hapa Life in Christ Ministries Zoe akiwa na maumivu ya miguu yaliyomsumbua kwa muda sasa, lakini wakati wa maombi ya kufunguliwa kwa pamoja (Mass Prayer au Mass deliverance) maombi yaliyoongozwa na Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph, dada Julieth aliweza kupokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.
Hapa dada yetu akiwa amekaa na akionekana ni mwenye maumivu.
Akimshukuru Mungu kwa kumponya.
Kutokana na maumivu aliyokuwa nayo ya mguu hakuweza kukimbia lakini hapa tunaona baada ya maombi aliweza kukimbia.
Yote yanawezekana kwake yeye aaminiye. Utukufu ni kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Hakika Mungu anashangaza sana kwa nguvu zake na miujiza yake,Mama Oliver alikuja akiwa na maumivu ya kiuno na mguu lakini naye alipokea uponyaji wake kupitia Mass Deliverance.
Hapa akishuhudia jinsi alivyopokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo.
Hapa akichuchumaa bila ya kuwa na maumivu ya aina yoyote.