TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 5 October 2014

TUMBO LILILOKUWA WAZI LAPONYWA KWA JINA LA YESU KRISTO

Mungu anaendelea kushangaza kwa ukuu wake dada Lisa John alikuja mwezi wa sita mwaka huu , tatizo lililomfanya afike katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe ni tatizo la tumbo kufumuka, Alilazwa katika hospital ya Amana jijini Dar es salaam ambako alikwenda kujifungua, alijifungua kwa oparesheni lakini kidonda hakikuweza kupona kila mara aliposhonwa tumbo lilifumuka. Ndipo alipoamua kumtafuta daktari wa madaktari Yesu Kristo wa Nazareth kwasababu yeye anaponya madaktari wanatibu. Hakika Mungu alionekana katika maisha ya dada yetu alifika na kuingia katika mstari wa uponyaji ( PRAYER LINE) ambayo hufanyika kila siku ya jumapili ikiongozwa na Roho Mtakatifu mwenyewe kwa kumtumia Mtumishi wake Prophet Joseph,mara mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alipomwekea mkono naye alipokea uzima kidonda kilifunga.

                               Hii ni picha inayoonyesha tumbo likiwa wazi na utumbo kuonekana.

        Dada Lisa akishuhudia matendo makuu ya Mungu aliyomtendea.Hapa akiwa ni mzima kabisa.
                 Prophet Joseph akimuombea kwa jina la Yesu Kristo uponyaji uendelee kudumu.
                           Nguvu ya Mungu ikimshukia dada Lisa.

                         Uponyaji na uzima wapatikana kwa Yesu Kristo. Isaya 53:5,Hakika kwa kupigwa kwake Yesu sisi tumepona Ahsante Yesu Kristo kwa uponyaji na uzima.







No comments:

Post a Comment