Hakuna kifungo ambacho Yesu hawezi kukifungua wala hakuna ngome Yesu asiyoweza kuivunja. Kaka David alikuwa kwenye kifungo cha ulevi wa bia ya Castle light kwa muda mrefu ndipo alipoamua kwamba lazima ulevi huu ufikie mwisho wake lakini si kwa nguvu zake maana kwa nguvu zake alikwisha shindwa kuacha ndipo alipoamua kutafuta mahali ambapo Yesu mtenda miujiza atamfungua, alifika kwenye huduma ya LIFE IN CHRIST MINISTRIES ZOE,na Yesu hakumpita alimfungua naye akawa huru kweli kweli. Kama anavyoonekana kwenye picha. Alikuja na pombe hii ili kuonyesha kwamba ni kweli amekuwa akiitumia pombe hii.
|
Kaka David akielezea huku akiwa ameshikilia pombe hiyo mkononi. |
Prophet Of God Prophet Joseph akimuombea ili kuondoa kiu yote ya pombe iliyomtesa kwa miaka mingi.