TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Saturday, 27 December 2014

YATUPASA KUSHUHUDIA NA KUSHUKURU KWA KILA JAMBO AMBALO YESU KRISTO ANATUTENDEA...

Ndugu yetu alifika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe kuja kushuhudia na kumshukuru Mungu kwa yale ambayo  Bwana wetu Yesu Kristo amewatendea katika maisha yao. Zaburi 9:1-2 inasema; Nitamshukuru Mungu kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu,nitafurahi na kukushangilia wewe,nitaliimba jina lako wewe uliye juu,ni vyema kumshukuru Mungu kwa kila jambo hata kama kwa macho ya nyama linaonekana ni dogo yatupasa kushukuru.

 Raji Jetha kutoka kunduchi alifika hapa Life in Christ Ministries Zoe, Nov.24/2014 akiwa amevunijka bega na alikuwa anatumia arm rest hata madaktari walimshauri kumwekea chuma maana haikuwa rahisi bega hilo kuunga lakini kwa neema ya Mungu shemeji yake aliweza kumleta katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe, wakati wa kipindi cha mass deliverance alipokea uponyaji. Alikwenda hospitali na kupiga X-ray na madaktari wakathibitisha hakika mkono umeunga kabisa. Na akaamua kurudi ili kushuhudia na kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyomtendea, hata madaktari waliachwa na maswali mengi kwa jinsi  ndugu Raji bega lilivyounga bila yakufanyiwa oparesheni yoyote. Hakika Yesu Kristo ni mponyaji mkuu.

                                                    Ndugu Raji Jetha katika picha.
                                  Akishuhudia jinsi alivyopokea uponyaji wa bega lake.
                                              Akimshukuru Mungu kwa kumponya.
Akienda kuketi, hakika amepokea uzima kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth...Hakuna jmbo gumu la kumshinda Mungu.











YESU KRISTO BADO ANAENDELEA KUUNGA MIFUPA

Hakika Mungu wetu ni mwaminifu tunazidi kuuona Ukuu wake kila iitwapo leo, maelfu wameendelea kufunguliwa na kuwekwa huru kutoka katika vifungo vya aina mbalimbali na Yesu Kristo mtenda miujiza.

Maria Ramadhani kutoka Yombo jijini Dar es salaam alikuja akiwa amevunjika mkono na hakuweza kuutumia mkono wake kufanya kazi yoyote lakini jinsi Mungu alivyomwaminifu wakati wa kipindi cha kufunguliwa kwa pamoja (Mass deliverance) dada Maria alipokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo mponyaji.


                                       Akishuhudia jinsi alivyopokea uponyaji.
 Akinyoosha mkono wake baada ya kupokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.
                                      Mkono ukiwa mzima kabisa kwa jina la Yesu Kristo.
                                              Aliweza kuukunja bila ya kusikia maumivu.
                  Akiugusa kuonyesha kuwa hakika  roho chafu ya maumivu imemwacha.
                                                   Akimshukuru Mungu kwa kumponya.



2. Aidano Mtui alipata ugonjwa wa kupooza (stroke) iliyopelekea ashindwe kutembea bila ya msaada wa fimbo, alifika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe akiwa anatembelea fimbo lakini wakati wa kipindi cha mass deliverance alifunguliwa naalitembea bila ya msaada wa fimbo hakika Yesu Kristo anaweza kuponya hata sasa.


                         Aidano Mtui akiwa katika nyumba ya Baba yetu wa Mbinguni. L.C.M Zoe.
                                            Akimtukuza Mungu kwa kumponya.
                                             Akitembea bila ya kutumia fimbo.
                          Prophet of God, Prophet Joseph akiwa na ndugu Aidano Mtui.

                       SIFA NA UTUKUFU NI KWA MUNGU WETU ALIYE JUU.