Hakika Mungu wetu ni mwaminifu tunazidi kuuona Ukuu wake kila iitwapo leo, maelfu wameendelea kufunguliwa na kuwekwa huru kutoka katika vifungo vya aina mbalimbali na Yesu Kristo mtenda miujiza.
Maria Ramadhani kutoka Yombo jijini Dar es salaam alikuja akiwa amevunjika mkono na hakuweza kuutumia mkono wake kufanya kazi yoyote lakini jinsi Mungu alivyomwaminifu wakati wa kipindi cha kufunguliwa kwa pamoja (Mass deliverance) dada Maria alipokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo mponyaji.
Akishuhudia jinsi alivyopokea uponyaji.
Akinyoosha mkono wake baada ya kupokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.
Mkono ukiwa mzima kabisa kwa jina la Yesu Kristo.
Aliweza kuukunja bila ya kusikia maumivu.
Akiugusa kuonyesha kuwa hakika roho chafu ya maumivu imemwacha.
Akimshukuru Mungu kwa kumponya.
2. Aidano Mtui alipata ugonjwa wa kupooza (stroke) iliyopelekea ashindwe kutembea bila ya msaada wa fimbo, alifika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe akiwa anatembelea fimbo lakini wakati wa kipindi cha mass deliverance alifunguliwa naalitembea bila ya msaada wa fimbo hakika Yesu Kristo anaweza kuponya hata sasa.
Aidano Mtui akiwa katika nyumba ya Baba yetu wa Mbinguni. L.C.M Zoe.
Akimtukuza Mungu kwa kumponya.
Akitembea bila ya kutumia fimbo.
Prophet of God, Prophet Joseph akiwa na ndugu Aidano Mtui.
SIFA NA UTUKUFU NI KWA MUNGU WETU ALIYE JUU.
No comments:
Post a Comment