TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Tuesday, 2 June 2015

UVIMBE WA MGUU WANYWEA KWA JINA LA YESU KRISTO

Anitha Machume alifika katika nyumba ya Mungu LCM Zoe akiwa amevimba mguu wake wa upande wa kulia. Alikuwa amepumzisha mwili alipoamka alikuta mguu wake umevimba , wakati wa ibada ya kufunguliwa kwa pamoja ( Mass deliverance) nguvu ya Mungu ilimchukua na kujikuta yuko chini. Mtumishi wa Mungu prophet Joseph alifika na kuamuru uvimbe na kila roho chafu kumwacha kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth na pale pale uzima uliingi ndani ya ndugu Anitha na akasimama na kutembea kawaida wakati mwanzo alikuwa akitembea kwa shida sana na pale pale uvimbe ukaanza kunywea. Kaka yake alipoona jinsi Mungu alivyomponya dada yake alishangaa matendo makuu ya Mungu na alimshukuru Mungu sana.

                              Mguu huo ulivyokuwa ukionekana kabla ya maombezi.
                            Ndugu Anitha akiwa ndani ya nyumba ya Mungu.
                      Akiwa chini mara baada ya kuchukuliwa na nguvu ya Mungu.
                       Prophet Joseph akimwombea kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
                        Akiwa chini na mguu ukiwa unonekana jinsi ulivyovimba.
                              Mara baada ya maombezi akitembea bila ya maumivu.
                                                 Akielezea alivyopokea uponyaji.
                         Kaka yake Anitha akimshukuru Mungu kwa kumponya dada yake.

                                             SIFA NA UTUKUFU WA MUNGU.

HAKUNA LINALOSHINDIKANA KWA BWANA

Godson Barnabas alifika katika nyumba ya Mungu, Life in Christ Ministries zoe akiwa na tatizo la ugonjwa wa moyo, mishipa ya moyo ilikuwa imepanuka na kusababisha kutokuweza kutembea bila ya msaada wa chuma cha kutembelea. Alipita kwenye mstari wa uponyaji na mtumishi wa Mungu prophet Joseph akamwekea mkono na nguvu ya ufufuo ikamponya ndugu Godson na kuwa huru kabisa.

                                  Ndugu Godson akiwa na fimbo kabla ya maombezi.
                                                Akiwa kwenye mstari wa uponyaji.
                        Prophet Joseph akifukuza roho ya udhaifu ndani ya ndugu Godson.
                                         Akisimama mara baada ya maombezi.
                                                  Akitembea bila ya msaada wa fimbo.

Ndugu Godson akiwa huru kabisa kutoka katika kila kifungo, hakuna linaloshindikana kwa Yesu Kristo wa Nazareth.