TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Monday, 10 August 2015

ROHO YA USHOGA YAMWACHA HURU KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Francis Moses amekuwa katika kifungo cha ushoga yapata miaka 9. Mama yake kwa upendo mkuu aliweza kumleta katika huduma ya Life in christ Ministries Zoe ili Bwana wetu Yesu Kristo aweze kumweka huru. Akiwa na umri wa miaka mitatu nduguzake waliamua kumchukua kutoka Dar es salaam na kwenda kuishi naye jijini Mbeya hii ni kutokana na kwamba mama yake mzazi hakuweza kumlea mara baada ya baba mzazi kufariki dunia.
Ndipo alipokuwa darasa la tatu alikwenda kuoga mtoni akiwa na kijana aliyemzidi umri, walipoanza kuoga yule kijana alianza kumshika mwili wake na ndipo alipomwingilia kinyume na maumbile bila ridhaa ya ndugu Francis. Tokea siku ile aliendelea na mchezo huo, ikafikia hatua ya kutokuweza kujizuia na kuendelea na mchezo huo wa kuingiliwa kinyume na  maumbile na wanaume tofauti tofauti. Akawa akivaa nguo za kike na hata kubadili mwondoko wake na kuwa kama mwanamke ilihali ni mwanaume. Wakati akiwa katika hali hiyo ya ushoga wanaume waliokuwa wakimwingilia walikuwa wakivunja uume wake ili usiweze kufanya kazi sawasawa, amekuwa katika hali hiyo kwa miaka 9. Pia alikuwa katika kifungo cha unywaji pombe na uvutaji ugoro. Kwa neema na upendo wa Mungu, prophet Joseph kwa kutumia jina la YESU Kristo aliweza kumfungua ndugu Francis kutoka katika kifungo hicho cha ushoga.

                                               Ndugu Francis katika picha.

                                            KABLA YA KUWEKWA HURU

                                          Hapa akionekana na suruali ya kike.
                                                  Akiwa na mama yake mzazi.
                                         Akielezea jinsi alivyojikuta katika hali hiyo.


                                               WAKATI WA KUFUNGULIWA
                  Prophet Joseph akiifukuza roho ya ushoga kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
                                       Roho chafu ya ushoga ikijidhihirisha.

                          Prophet Joseph akiamuru uume wa ndugu Francis urudi kuwa sawa.

                   Familia ya wana Zoe wakimtukuza Mungu kwa kumweka ndugu Francis huru.

                                       MARA BAADA YA KUWEKWA HURU
 Hivi ndivyo anavyoonekana baada ya kuwa huru kutoka katika roho chafu ya ushoga.
                                           Akiwa nadhifu na mavazi ya kiume.

                              WIKI MOJA BAADA YA KUWEKWA HURU.

Wiki moja baada ya kuwekwa huru alifika katika nyumba ya Mungu kumshukuru Mungu kwa kumtoa katika roho chafu ya ushoga. 

Katika Wagalatia 5:16-18 inasema; " basi nasema enendeni kwa Roho wala hamtatimiza kamwe tamaa za mwili. 17. Kwasababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. 18. Lakini mkiongozwa na Roho hampo chini ya sheria.

                   Hakika yatupasa kuenenda katika roho ili adui asitutege.

                                                    UTUKUFU KWA BWANA.

No comments:

Post a Comment