TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Monday, 9 February 2015

KWA KUSIKIA NENO LENYE UZIMA WAPOKEA UPONYAJI

Zaburi 107: 20 inasema, Hulituma neno lake, huwaponya, huwatoa katika maangamizo yao.

Hakika tumemuona Mungu akimtumia mtumishi wake, prophet Joseph kwa namna ya tofauti kabisa kuunga mifupa na kuwaponya watu. Katika ibada ya jumapili 8/2/2015 maelfu walipokea uponyaji kupitia neno alilokuwa akifundisha mtumishi wa Mungu Prophet Joseph, neno lililokuwa na nguvu ya Mungu, ya kwamba sisi kama wakristo hatupaswi kuumwa wala kuugua kwasababu tuna maisha ya Mungu ndani yetu. kwa kufundisha tu neno hili mifupa iliyokuwa imevunjika iliiunga .

                    Baadhi ya maelfu waliopokea uponyaji mara baada ya kusikia neno lenye uzima.

HAKIKA MANABII WA KWELI WANAZUNGUMZA BADALA YA MUNGU


Manabii wa kweli , walioitwa na Mungu hawazungumzi maneno yao wenyewe bali hunena yale yaliyotoka kwa Bwana.
Mrs. Humfrey alifika katika nyumba ya Mungu Zoe, kushuhudia yale ambayo Mungu ameyatenda katika maisha yake na familia yake. Miaka michache iliyopita walifika yeye na mumewe katika hududma ya LCM mara ya kwanza walipofika walipata neema ya kusikia neno la kinabii kutoka kwa Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph. Neno hilo lilikuwa maalum kwa ndugu Humfrey, mtumishi wa Mungu Prophet Joseph akiongozwa na Roho Mtakatifu alimweleza ndugu Humfrey kuwa ni lazima awe makini maana anamuona akiwa kwenye wheelchair. Hakika manabii wanaposema ni lazima tuwe watii kwa kila neno watakalolinena, pindi ndugu Humfrey alipopata neema hiyo ya kusikia kutoka kwa Mungu kupitia kwa Prophet Joseph hakulitii neno lile. Alipata neema ya kwenda nchini Marekani alipofika kule akawa kwenye mahusiano na mwanamke mwingine kinyume na mpango wa Mungu, alirudi nchini na baada ya kipindi kifupi yule mwanamke alikuja nchini Tanzania, na bila kumweleza mke wake walikwenda mkoani mbeya waliporudi Dar es salaam hakika kama prophet Joseph alivyotoa neno la kinabii, neno lile lilitimia aliporudi tu alipooza na kuanza kutumia wheel chair. Kwa neema ya Mungu kabla ya kwenda nyumbani (Mbinguni) aliweza kurekebisha na mke wake, ndipo kwa upendo mkuu Mungu Baba alimwita ndugu yetu Humfrey nyumbvani kwa amani kabisa. Habari zaidi soma kwenye ukurasa wetu wa facebook.

Mrs. Humfrey akimshukuru na kumtukuza Mungu kwa mambo yote aliyomtendea.

                     Hakika yatupasa kusikia na kutii yale manabii wanayotueleza.