Kama tunavyoona katika picha hizi.
Ndugu Francis anaonekana akiwa anatembea bila y amsaada wa magongo.
Hapa akishuhudia baada ya kupokea uponyaji.
Mke wa ndugu Francis akimshukuru Mungu kwa uponyaji.
Hakika Yesu Kristo anaendelea kuponya hata sasa haijalishi ugonjwa,tatizo ulilonalo ukiamini tu kwamba Uzima wapatikana kwake hakika atakuponya.
Pia ndugu yetu Yohana Meshack alikuja akiwa na maumivu ya miguu na kiuno kwa wiki mbili naye alikuja akiwa anatembelea magongo lakini alipokea uponyaji wake na kuwa mzima kabisa.
Akitembea bila ya kutumia gongo.
Akishuhudia kwa kuponywa na Bwana wetu Yesu Kristo.
Hili ndilo gongo alilokuwa anatumia kutembelea akiwa amelitupa kuonyesha kuwa ni kweli amepona.
Mtenda kazi wa Life in Christ Ministries Zoe akilitundika gongo hilo katika ukuta wa uponyaji ikiwa ni ishara kuwa ndugu yetu ni mzima na haihitaji tena kutembelea gongo hilo.
Sifa kwa Bwana wetu Yesu Kristo.!!!
No comments:
Post a Comment