TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Saturday, 14 June 2014

FIGO ZILIZOKUWA ZIMEKUFA ZAPONYWA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Hakuna ugonjwa ambao ni mkubwa kuliko jina la Yesu Kristo wa Nazareth, kwa kutaja jina hili lenye nguvu kupita majina yote kila ugonjwa unaondoka ndivyo ilivyokuwa kwa dada Beatrice aliyekuwa akisumbuliwa na figo kwa muda mrefu, ambapo figo zake zote mbili zilikuwa haziwezi kufanya kazi sawa sawa na kusababisha hadi kushindwa kujisaidia haja ndogo kwa urahisi. Alipelekwa hospitalini na kuwekewa dripu 36 lakini hakupata nafuu yoyote na pia hakuweza kula hata chakula kwa takribani wiki mbili, ndipo alipoamua kuja  Life in Christ Ministries Zoe ili akutane na Yesu Kristo mtenda miujiza kwa kumtumia Prophet Joseph. Jumapili ya tarehe 1/8/2014 alifika akiwa hajiwezi kabisa kama ambavyo anaonekana kwenye picha.













Alikuja akiwa na maumivu makali sana yaliyopelekea hata ashindwe kufanya kazi yoyote.

         Prophet Joseph akiamuru kila aina ya roho wa  maumivu kumwachia dada Beatrice.

                       Nguvu ya Mungu ikifanya kazi ya kuondoa kila aina ya roho wa maumivu.
 Dada Beatrice akimshukuru Mungu baada ya roho wa maumivu kumwacha kwa jina la Yesu      Kristo wa Nazareth.
                   Watu wakimshukuru Mungu kwa uponyaji wa dada Beatrice.

 Baada ya kuondolewa roho wa maumivu ndipo ilipofuata awamu ya pili ya kuponywa figo zake zote na Yesu Kristo kupitia Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph.








 Prophet Joseph akimwombea kwa kutumia jina la Yesu Kristo wa Nazareth ambaye kwake kila ugonjwa unatii.





 Baada ya maombi Prophet Joseph akimwamuru kusimama maana alikuwa tayari ameshapokea uponyaji wake.




                        Dada Beatrice akimshukuru Mungu kwa kumpatia figo mpya .

            Akilia kwa furaha na kumshukuru Mungu kwa kumrejeshea uhai katika figo zake.
                             Prophet Joseph akiwa na dada Beatrice.


 Akitoa ushuhuda wa kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyomtendea katika maisha yake,hapa akiwa mwenye furaha na nguvu tele baada ya uponyaji, maana haikuwa rahisi kwake hata kusimama na kuongea kabla ya uponyaji lakini baada ya uponyaji anaonekana akiwa amesimama na kuongea akiwa na nguvu tele.




                Maelfu ya watu waliokusanyika wakimtukuza Mungu kwa uponyaji huu.

Hatimaye baada ya kukaa wiki mbili bila ya kula baada ya maombi aliweza kusikia njaa na kuweza kula.



Hakika hakuna ugonjwa wowote ambao una nguvu kupita jina la Yesu Kristo, dada Beatrice alikuja akiwa hajiwezi kabisa lakini kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth kila kilichokuwa kimekufa ndani ya mwili wake kilifufuliwa na Yesu Kristo ambaye kwa jina lake kila aina ya mateso yanaondolewa. Mungu anaendelea kutenda hata sasa tunachotakiwa ni kuamini tu!!!