Kati ya maelfu waliofika katika ibada waliweza kukutana na Yesu Kristo mtenda miujiza na kuponywa na kufunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali hawa ni baadhi yao tu. Kama ambavyo tunaona kwenye picha hapa chini.
Dada yetu alifika hapa LCM akiwa na tatizo la kutokusikia na alikuwa hawezi kutembea lakini aliweza kupata uponyaji wa hapo hapo (Instant Healing) kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth wakati wa kufunguliwa kwa pamoja (Mass Deliverance) akaweza kutembea na kusikia.
Hapa akiwa mwenye furaha tele baada ya kuweza kutembea na kusikia.
Ndugu yetu bwana Dondi Dondi Faraji kutoka Kigoma, alikuwa na matatizo ya pingili za mgongo kuuma hakuweza kuinama wala kuchuchumaa lakini mara baada ya maombi ya Maa deliverance yaliyoongozwa na Prophet Joseph akiongozwa na roho aliweza kupata uponyaji wake hapo hapo.
Hapa akionyesha kwamba ni kweli maumivu yote yamemwacha.
Hapa akiwa amechuchumaa bila ya kuwa na maumivu yoyote.
Dada yetu Fatma Ally alikuwa amepoteza siku zake kwa miezi 6 pindi Prophet Joseph alipoongoza maombi ya kwamba watu wasiopata siku zao wapate kwa jina la Yesu Kristo wapate dada Fatma akapata siku zake hapo hapo,hapa akionekana mwenye furaha tele baada ya kuponywa na Yesu Kristo.
Dada yetu alikuja akiwa hawezi kuembea kama anavyoonekana hapa.
Baada ya maombi hapa akiwa nasimama bila ya kutumia fimbo au msaada wa mtu.
Hapa akitembea mwenyewe bila kushikiliwa au kutumia fimbo aliyokuja nayo.
Yesu Kristo hakusema kwamba ameacha kuponya anaendelea kuponya hata sasa... Hallelujah sifa na heshima zina yeye Mungu wetu .