Ellylumba Mshana alikuja akiwa anatembelea kifaa maalum cha kutembelea kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo, presha pamoja na maumivu makali kwenye magoti yake kwa zaidi ya miaka 20, amekwenda kwenye hospitali nyingi lakini tatizo lilikuwa palepale. Alifika katika nyumba ya Mungu LCM akiamini kabisa kuwa sasa ni wakati wa Mungu kumponya na ndivyo ilivyokuwa, Mungu hakumwacha alimponya na kuwa huru kabisa.
Akishuka kwenye usafiri uliomleta.
Akiingia kwenye nyumba ya Mungu. LCM Zoe.
Akitembea kwa kutumia kifaa maalum.
Akilia kwa furaha mara baada ya kupokea uponyaji.
Akitembea bila ya msaada wa kifaa cha kutembelea.
Mungu wetu ni Mungu atendaye hata sasa.
Thursday, 2 April 2015
MKONO ULIOVUNJIKA WAUNGA
Kila jumapili Mungu anaendelea kumtumia mtumishi wake, Prophet Joseph kwa ishara, maajabu na miujiza. Jumapili hii tuliweza kushuhudia miujiza mingi ya kushangaza kutoka kwa Yesu Kristo kupitia Prophet Joseph. Ndugu Hashim Jumanne alipata ajali ya pikipiki na kusababisha mfupa katika mkono wake kuvunjika, alipokwenda hospitali madaktari walimwekea chuma na hogo ili mfupa wake uweze kuunga, Kwa neema ya Mungu alisikiliza neno lililokuwa likifundishwa na prophet Joseph neno lenye uvuvio wa Roho Mtakatifu na kwa kuamini tu mkono uliunga papo hapo.
Ndugu Hashim pichani.
Akiwa akiingia katika nyumba ya Mungu tayari kupokea uponyaji wake.
Ndugu. Hashi akiwa kwenye nyumba ya Mungu.
Akishuhudia jinsi alivyopokea uponyaji.
Akinyosha juu mkono kuonyesha kuwa maumivu yameshamwacha.
Hiki ni kifaa alichokuwa amekiweka mkononi ili kushikizia hogo mara baada ya maombi alikitupa kuonyesha kuwa hakika amekwisha kuwa mzima.
Baada ya kutoa P.O.P .
Ndugu Hashim pichani.
Akiwa akiingia katika nyumba ya Mungu tayari kupokea uponyaji wake.
Ndugu. Hashi akiwa kwenye nyumba ya Mungu.
Akishuhudia jinsi alivyopokea uponyaji.
Akinyosha juu mkono kuonyesha kuwa maumivu yameshamwacha.
Aliweza kukunja mkono mara baada ya kupokea uponyaji.
Hiki ni kifaa alichokuwa amekiweka mkononi ili kushikizia hogo mara baada ya maombi alikitupa kuonyesha kuwa hakika amekwisha kuwa mzima.
P.O.P likiondolewa katika mkono wake mara baada ya uponyaji . Halihitaji tena maana si sehemu ya maisha yake.
Baada ya kutoa P.O.P .
AACHA MAGONGO KWA NENO LA MUNGU LENYE NGUVU YA KUPONYA...
Lydia Mwaipopo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kushindwa kutembea kwa muda wa miaka zaidi ya 15 hakika nguvu ya Mungu ina uwezo wa kuponya bila ya kuwekewa mkono ukiamini tu Mungu anakugusa, wakati mtumishi wa Mungu prophet Joseph alipokuwa akifundisha dada Lydia alishikwa na haja na akiwa anaelekea chooni(Toilet) huku akitembea na magongo, nguvu ya Mungu yenye kuponya ilimgusa na akawa huru kabisa kutoka kwenye mateso ya kutembelea magongo. Hakika kwa neno la mafunuo tu dada Lydia aliweza kupokea uponyaji wake na akaweza kutembea pasipo magongo. Alikwenda sehemu mbalimbali hakuweza kupata uponyaji lakini wakati wa Bwana kumweka huru ulipofika hakuna kilichoweza kuzuia.
Lydia Mwaipopo kama ambavyo anaonekana pichani.
Akishuka kwenye pikipiki iliyomleta.
Akiingia kwenye nyumba ya Mungu, Life in Christ Ministries Zoe.
Hapa akiwa anatokea chooni huku akiwa hana mgongo, pembeni ni afisa muuguzi na mtenda kazi katika nyumba ya Mungu .
Akitembea bila ya msaada wa magongo.
Akimshukuru Mungu kwa kumponya.
MUNGU WETU ANATENDA HATA SASA.
Lydia Mwaipopo kama ambavyo anaonekana pichani.
Akishuka kwenye pikipiki iliyomleta.
Akiingia kwenye nyumba ya Mungu, Life in Christ Ministries Zoe.
Hapa akiwa anatokea chooni huku akiwa hana mgongo, pembeni ni afisa muuguzi na mtenda kazi katika nyumba ya Mungu .
Akitembea bila ya msaada wa magongo.
Akimshukuru Mungu kwa kumponya.
MUNGU WETU ANATENDA HATA SASA.