Lydia Mwaipopo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kushindwa kutembea kwa muda wa miaka zaidi ya 15 hakika nguvu ya Mungu ina uwezo wa kuponya bila ya kuwekewa mkono ukiamini tu Mungu anakugusa, wakati mtumishi wa Mungu prophet Joseph alipokuwa akifundisha dada Lydia alishikwa na haja na akiwa anaelekea chooni(Toilet) huku akitembea na magongo, nguvu ya Mungu yenye kuponya ilimgusa na akawa huru kabisa kutoka kwenye mateso ya kutembelea magongo. Hakika kwa neno la mafunuo tu dada Lydia aliweza kupokea uponyaji wake na akaweza kutembea pasipo magongo. Alikwenda sehemu mbalimbali hakuweza kupata uponyaji lakini wakati wa Bwana kumweka huru ulipofika hakuna kilichoweza kuzuia.
Lydia Mwaipopo kama ambavyo anaonekana pichani.
Akishuka kwenye pikipiki iliyomleta.
Akiingia kwenye nyumba ya Mungu, Life in Christ Ministries Zoe.
Hapa akiwa anatokea chooni huku akiwa hana mgongo, pembeni ni afisa muuguzi na mtenda kazi katika nyumba ya Mungu .
Akitembea bila ya msaada wa magongo.
Akimshukuru Mungu kwa kumponya.
MUNGU WETU ANATENDA HATA SASA.
No comments:
Post a Comment