TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Saturday, 13 December 2014

KUFUNGULIWA KUTOKA KATIKA KIFUNGO CHA ULEVI

Dada Evelyn Mkingilima alikuja katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe kutaka msaada kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo wa kumtoa katika kifungo cha ulevi wa kupindukia, amekuwa katika kifungo cha ulevi wa kunywa mizinga ya konyagi kwa muda mrefu amekuwa akinywa hata mizinga 10 ya konyagi kwa siku, alijaribu kuacha kwa nguvu zake mwenyewe lakini haikuwezekana ndipo aliamua kumtafuta mwenye nguvu kuliko wote ambaye ni Yesu Kristo Mkombozi wetu ambaye kwake yeye hakuna kinachoshindikana. Kwa kumtumia mtumishi wake Prophet Joseph, dada Evelyn aliwekwa huru na Yesu Kristo mtenda miujiza.

                                 Akiwa ameshikilia pombe aina ya konyagi.
                       Akinywa kuonyesha ni kweli alikuwa anatumia pombe hiyo.
               Roho chafu ya pombe ikifukuzwa na prophet Joseph kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
                                            Nguvu ya Mungu ikiwa imemchukua.
                                  Baada ya kuwekwa huru hakuweza kuinywa pombe hiyo.
Akiwa ametema pombe hiyo, maana baada ya kuwekwa huru alisema ile hamu ya kunywa pombe hiyo ya konyagi imemwacha kabisa. Utukufu kwa Bwana.

AFUNGULIWA KUTOKA KATIKA KIFUNGO CHA KULA NYAMA MBICHI NA KULA CHUMVI

Erica Katunzi amekuwa kwenye kifungo cha kula nyama mbichi kwa zaidi ya miaka 10 na pia alikuwa kwenye kifungo cha kula chumvi, alikuwa hawezi kula nyama iliyopikwa alikuwa anakula nyama ya ng'ombe,kuku vyote vikiwa ni vibichi. Kabla ya kufunguliwa aliweza kuonyesha ni kwa kiasi gani ibilisi amemwonea kwa kumfanya ale chumvi na nyama mbichi, pia alisema kuwa hupandwa hasira pale mtu anapomnyang'anya nyama hiyo hata huhisi kumkamata mtu huyo na kumla. Hata ikapelekea watu wanaomfahamu kumdhania kuwa ni mchawi kutoka na kula nyama mbichi. Lakini Mungu ni mwema na mwaminifu sana dada yetu alifika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe, na akafunguliwa na Yesu Kristo wa Nazareth kupitia mtumishi wake Prophet Joseph.

Hapa akielezea mateso anayoyapata na akiwa ameshikilia mfuko wenye nyama mbichi.

                                                    Akiwa na nyama mbichi mkononi.
                                                         Akila nyama hizo mbichi.
                      Mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph akimfungua kwa jina la Yesu Kristo.

                          Nguvu ya Mungu ikiwa imemchukua na kufukuza roho chafu.


                        BAADA YA KUWEKWA HURU NA YESU KRISTO WA NAZARETH.
                       Baada ya kuwekwa huru hakuweza kula tena nyama mbichi.


Akijaribu kuonja chumvi nayo hakuweza kuila tena hii ikionyesha hakika Yesu Kristo anaendelea kufungua watu hata sasa . Hakuna kifungo ambacho Yesu Kristo hawezi kukifungua unachotakiwa ni kuamini tu. Asante Yesu Kristo.





.