TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 14 September 2014

UTI WA MGONGO WAKAA SAWA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Dada Irene William alikuja kushuhudia matendo makuu ambayo Mungu alimtendea, alikuja akiwa na tatizo la miguu ambalo lilisababishwa na tatizo la uti wa mgongo, tattizo hili lilisababisha awe na maumivu makali ambayo yalisababisha ashindwe kusimama kwa muda mrefu na kushindwa kutembea kwa muda mrefu,lakini jumapili ya tarehe 24/8/2014 alisoma Yohana 10:10 inayosema  Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Mara alipoamini na kukiri neno hili alipokea uzima wake kutoka kwa Yesu Kristo.
Dada Irene akiwa ameshikilia mkononi lumbar corset au mkanda maalum uliokuwa ukimsaidia wakati akiwa na maumivu.
                Mume wake dada Irene akimshukuru Mungu kwa kumponya mke wake.
                      Dada Irene akiwa na mumewe wakimshukuru Mungu.

Akiiweka Lumbar Corset kwenye ukuta wa uponyaji ikiwa ni ishara kuwa haihitaji tene kuvaa mkanda huo kwa kuwa ameshapokea uponyaji wake.

Hakika Yesu Kristo anaendelea kutenda hata sasa hakusema kuwa hakutakuwa na uponyaji au kufunguliwa La hasha! bado anaponya hata sasa ukiamini tu atakuponya nawe utakuwa mzima kabisa haijalishi ugonjwa au mateso gani unayo akisema imekwisha amini kuwa imekwisha. Ahsante Yesu kristo!!!

MAUMIVU YA SIKIO YAONDOLEWA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Dada Esther Njeri kutoka nchini Kenya alikua akiwa na maumivu katika sikio na pia sikio lililkuwa linatoa usaha ilimbidi kila mara atumie kitambaa kufuta usaha, mara baada ya maombi alipokea uponyaji wake na pia alitoa ushuhuda kuwa alikuja mwaka jana akiwa na tatizo la mimba kutoka kila alipopata ujauzito mimba ilitoka lakini mara baada ya kuja Zoe na kupata maombi ameweza kupata neema ya kupata ujauzito na kujifungua bila ya kuwa na tatizo lolote na alijifungua mtoto aitwaye Imani.


Dada Esther akishuhudia matendo makuu ambayo Mungu amemtendea.
UTUKUFU KWA MUNGU!!!

KUFUNGULIWA KWA PAMOJA (MASS DELIVERANCE)

Kila siku ya ibada tunazidi kumwona Mungu akiwafungua watu na kutenda miujiza mbalimbali, hakika Mungu tunayemtumikia sio wa kawaida. Katika ibada ya jumapili 14/9/2014 Mungu aliwafungua watu mbalimbali kupitia mtumishi wake Prophet Joseph.


Baadhi ya maelfu waliofika ktika huduma ya Life in Christ Ministries Z.oe wakiwa wamechukuliwa na nguvu ya Mungu,nguvu iletayo afya,uzima na kufunguliwa kutoka katika mikono ya ibilisi