TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Monday, 19 January 2015

APOKEA UPONYAJI MARA TU BAADA YA KUSIKIA NENO LA UZIMA.

Katika Biblia Takatifu, kitabu cha Warumi 10:17 inasema " Imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo".

Katika ibada ya jumapili 18/1/2015 mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alikuwa akifundisha juu ya maisha ya Mungu ndani yetu (ZOE) na kusema kuwa pindi mtu anapopata neema ya kuwa na maisha ya Mungu ndani yake magonjwa yanakuwa si sehemu yake. Ndugu Francis Mwaluwanda aliyekuwa amepata ajali, baada ya pikipiki aliyopanda kugongwa na daladala uso kwa uso na kusababisha mfupa wa mguu wake kuvunjika na alipokwenda hospitali ya Sinza na Mwananyamala kote ilishindikana na akahamishiwa katika hospitali ya Muhimbili, pindi alipolisikia neno la uzima lililokuwa likifundishwa na mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph juu ya maisha ya Mungu ndani yetu, ndugu Francis uzima uliingia katika mguu wake palepale na kupokea uponyaji wa mguu maana alikuja akiwa anatembelea magongo lakini mara baada ya kulisikia neno la uzima lenye uvuvio wa Roho Mtakatifu aliweza kusimama bila ya kutumia magongo.
 Kwa kuthibisha kama ni kweli mfupa wake ulikuwa umevunjika kwa utukufu wa Mungu, Afisa wa afya kutoka wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam alikuja kusoma X ray ya ndugu Francis na kuthibitisha ni kweli ndugu Francis mfupa wake ulikuwa umevunjika. Na ndugu Francis alitakiwa kufanyiwa upasuaji  tarehe 19/1/2015 katika hospitali ya Muhimbili kitengo cha mifupa MOI ili kumwekea vyuma kama antenna.
Lakini kwa uaminifu wa Mungu alipokea uponyaji na kutupa magongo na akatembea bila ya msaada wa magongo kwavile magongo si sehemu ya maisha yake.



                                 Ndugu Francis akishuhudia matendo makuu ya Mungu.
                  Ndugu zake na ndugu Francis wakishuhudia matendo makuu ya Mungu.
                                                       X -ray ya ndugu Francis.
                             Ndugu Francis akikimbia bila ya kuwa na maumivu ya aina yoyote.

 Ndugu wakitokwa na machozi ya furaha baada ya kuona jinsi ambavyo Bwana Yesu Kristo amemponya ndugu yao.
                                  Magongo yakitundikwa juu kwa ajii ya ushuhuda.

                         Magongo si sehemu ya ndugu Francis yanabaki kuwa ushuhuda tu.

                                           JINA LA BWANA LIBARIKIWE.

FANGASI ZA MUDA MREFU ZAKOMA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Kwa miaka 11 dada Dorice Georvine ameteseka na fangasi za sehemu za siri lakini kwa neema ya Mungu alifika katika nyumba ya Mungu Life in Christ Ministries Zoe,ili aweze kupokea uponyaji kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Fangasi hizi ziliharibu mfumo wake wa mayai,alipokwenda hospitalini alipewa dawa lakini hazikumsaidia,pia fangasi hizi zilisababisha hata asiweze kupata ujauzito, pia kutokana na fangasi hizo alimbidi kuvaa nguo za ndani mbili,pedi au vitambaa kutokana na kutokwa na maji sehemu zake za udada maji yenye harufu kali. Mara baada ya kufunguliwa Prophet Joseph aitoa neno la kinabii kwa Dorice ya kwamba kuanzia sasa maji yaliyokuwa yakimtoka sehenu zake za udada hayatamtoka tena na aende chooni akajikague hakika alipokwenda kujikagua akakuta hakuna maji yoyote yaliyokuwa yanamtoka, maji yenye harufu yalikoma palepale kwa jina la Yesu Kristo mtenda miujiza.

                                                 Pichani ni dada Dorice.
                                               Akielezea kuhusu fangasi hizo.
 Prophet Joseph akiamuru kila roho chafu ya fangasi kumwacha dada huyu kw ajina la Yesu Kristo wa Nazareth.
 Akimshukuru Yesu Kristo kwa kumweka huru, huku akielekea chooni kujikagua.

Hiki ni kitambaa ambacho alikuwa akikiweka sehemu ya udada ili kuzuia maji yaliyokuwa yakimtoka lakini kwa utukufu wa Mungu, alipokwenda kujikagua akakuta maji yale hayatoki tena kama alivyokuwa ametoa neno la kinabii mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph.

Hakuna ugonjwa ambao Yesu Kristo hawezi kuuponya. Libarikiwe jina la Yesu Kristo.







AFUNGULIWA KUTOKA KATIKA KIFUNGO CHA KUNYWA MAFUTA YA TAA NA KUTAFUNA HELA...

Nguvu za Mungu za kuwatoa watu kutoka katika vifungo vya aina mbalimbali zinaendelea kuonekana hata sasa. Hakika tunakila sababu ya kumtukuza Mungu.
Agness Richard alikuwa kwenye kifungo cha kunywa mafuta ya taa na kutafuna hela za noti kwa miaka 7. Mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema kuwa anachikiona kwa dada huyu ni zaidi ya kunywa mafuta ya taa,na kwamba pia dada Agness alikuwa na tatizo katika ubongo wake amayo humletea hali ya kuchanganyikiwa, ndipo mtumishi wa Mungu prophet Joseph akielekezwa na RohoMtakatifu alisema dada huyu atafunguliwa mara mbili kwanza ni kutoka katika kifungo cha kunywa mafuta ya taa na kutafuna hela na kufunguliwa kwa mara ya pili ni kutoka katika hali ya kuchanganyikiwa.


                                                   Mafuta ya taa aliyokuja nayo.

                                  Dada Agnes akiwa ameshikiliwa chupa ya mafuta ya taa.

Mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph akiongozwa na Roho Mtakatifu akaendelea kusema kuwa hali hii inampata dada huyu akiwa kwenye siku zake ndipo dada Agnes alipokiri kuwa ni kweli hali hii humtokea akiwa katika siku zake.
    Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph akimfungua dada Agness kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.

Pia mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alisema mpango aliokuwa nao adui kwa dada Agness ni kumpa kansa ya tumbo lakini mara baada ya maombi,prophet Joseph alitoa neno la kinabii ya kwamba dada Agness hatakaa apate kansa ya tumbo kamwe kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.


                Hapa Prophet Joseph akitumia jina la Yesu Kristo kumweka huru kutoka katika hali ya kuchanganyikiwa.

Dada Agness akimshukuru Yesu Kristo wa Nazareth kwa kumweka huru kutoka katika vifungo vyote vya adui.

Mwanzo 18:14- inasema; Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? Hakika hakuna neno gumu la kumshinda Bwana tumeendelea kuona nguvu za Mungu zikiwatoa watu kutoka katika vifungo vya aina zote, Hakika Yesu Kristo ni Bwana wa Mabwana.

                                           Utukufu kwa Yesu Kristo wa Nazareth.