Katika ibada ya jumapili 18/1/2015 mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alikuwa akifundisha juu ya maisha ya Mungu ndani yetu (ZOE) na kusema kuwa pindi mtu anapopata neema ya kuwa na maisha ya Mungu ndani yake magonjwa yanakuwa si sehemu yake. Ndugu Francis Mwaluwanda aliyekuwa amepata ajali, baada ya pikipiki aliyopanda kugongwa na daladala uso kwa uso na kusababisha mfupa wa mguu wake kuvunjika na alipokwenda hospitali ya Sinza na Mwananyamala kote ilishindikana na akahamishiwa katika hospitali ya Muhimbili, pindi alipolisikia neno la uzima lililokuwa likifundishwa na mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph juu ya maisha ya Mungu ndani yetu, ndugu Francis uzima uliingia katika mguu wake palepale na kupokea uponyaji wa mguu maana alikuja akiwa anatembelea magongo lakini mara baada ya kulisikia neno la uzima lenye uvuvio wa Roho Mtakatifu aliweza kusimama bila ya kutumia magongo.
Kwa kuthibisha kama ni kweli mfupa wake ulikuwa umevunjika kwa utukufu wa Mungu, Afisa wa afya kutoka wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam alikuja kusoma X ray ya ndugu Francis na kuthibitisha ni kweli ndugu Francis mfupa wake ulikuwa umevunjika. Na ndugu Francis alitakiwa kufanyiwa upasuaji tarehe 19/1/2015 katika hospitali ya Muhimbili kitengo cha mifupa MOI ili kumwekea vyuma kama antenna.
Lakini kwa uaminifu wa Mungu alipokea uponyaji na kutupa magongo na akatembea bila ya msaada wa magongo kwavile magongo si sehemu ya maisha yake.
Ndugu Francis akishuhudia matendo makuu ya Mungu.
Ndugu zake na ndugu Francis wakishuhudia matendo makuu ya Mungu.
X -ray ya ndugu Francis.
Ndugu Francis akikimbia bila ya kuwa na maumivu ya aina yoyote.
Ndugu wakitokwa na machozi ya furaha baada ya kuona jinsi ambavyo Bwana Yesu Kristo amemponya ndugu yao.
Magongo yakitundikwa juu kwa ajii ya ushuhuda.
JINA LA BWANA LIBARIKIWE.
No comments:
Post a Comment