TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Tuesday, 10 February 2015

MKONO WAKAA SAWA KWA NENO LA UPONYAJI

Rose Richard kutokea Kibamba aliweza kupokea uponyaji wake kupitia neno lililokuwa likifundishwa na mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph, na mkono wake kuunga kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.

                                            Rose Richard pichani akiwa na P.O.P mkononi.

                                           Prophet Joseph akiwa na Rose Richard.
                            Rose akishuhudia jinsi alivyopokea uponyaji wa mkono wake.
                        Mama yake Rose akimshukuru Mungu kwa kumponya mtoto wake.

Prophet Joseph akiwa na mtoto Rose, huku kamba ya P.O.P ikiwa chini mara baada ya kupokea uponyaji wake.

KWA NENO LA UZIMA MFUPA WA MGUU WAUNGA

Mahmud Juma alikuja akiwa anatembelea magongo kutokana na mfupa wa mguu wake kuvunjika na kuweka vyuma, lakini kwa neema ya Mungu mara tu baada ya kusikia neno la uponyaji ndugu Mahmud alipokea uponyaji wake papo hapo. Utukufu kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

                            Ndugu Mahmud akiwa katika nyumba ya Mungu, LCM ZOE.

                        Mara baada ya kusikia neno akitembea bila ya msaada wa magongo.
                                               Akikanyaga bila ya tatizo lolote.



                      Hivi ndivyo mguu wa ndugu Mahmud unavyoonekana ukiwa na chuma.

MKONO WAUNGA MARA BAADA YA KUSIKIA NENO LA UZIMA

Israel M kutokea Kigoma aliweza kupokea uponyaji wa mkono wake uliokuwa umevunjika mara baada ya kusikia neno lenye uzima kutoka kwa mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph, alikuja akiwa amefunga mkono wake mara baada ya kupokea uponyaji huo mkono haukuwa na maumivu yoyote na uliunga palepale.

                                          Ndugu Israel akiwa kwenye nyumba ya Mungu.

                            Akielezea jinsi alivyoelewa somo la uzima wa Mungu ndani yetu.
    Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph akiondoa kifaa hicho katika mkono wa ndugu Israel.
                                           Akiwa huru baada ya kupokea uponyaji.
                                                Akishuhudia matendo makuu ya Mungu.

                            Kifaa hicho kikiwa chini mara baada ya kupokea uponyaji.
Kifaa hicho kikitundikwa kwa ajili ya ushuhuda na ikionyesha kuwa ndugu Israel ni mzima na haihitaji kukivaa kifaa hicho tena kwa utukufu wa Mungu.
Hivi ndivyo kinavyoonekana kikiwa juu kwa ajili ya ushuhuda kuwa hakika Mungu anaweza kuponya na kuunga kila aina ya mfupa.