Dada yetu Jaquline Kaaya alipata neema ya kupokea neno la kinabii kutoka kwa Prophet Joseph, mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alimweleza kuwa mara nyingi dada huyu amekuwa akiota anahesabu fedha nyingi na mara kwa mara amekuwa akipoteza fedha katika mazingira yasiyoeleweka dada Jaquline akakiri kuwa hakika ni kweli ndipo mtumishi wa Mungu Prophet Joseph akamwambia kuanzia sasa hatapoteza hela tena na ameshuhudia ni kweli toka apate neno hilo la kinabii hajapoteza tena pesa. Na pia aliendelea kushuhudia matendo makuu ambayo Mungu amemtendea alikuwa ana uvimbe kwenye ziwa lake lakini alipopita katika mstari wa uponyaji (prayer line) uvimbe ulipotea kwa jina la Yesu Kristo na ni mzima kabisa.
Jaquline Kaaya akishuhudia jinsi Mungu alivyomtendea. UTUKUFU KWA YESU KRISTO WA NAZARETH.
Venitha Joseph Mungu amemponya mguu wake wa kulia alikuja akiwa na maumivu na alikuwa ameshonwa . Lakini alipofika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe, Yesu Kristo mtenda miujiza aliweza kumponya wakati wa kipindi cha Mass deliverance (kufunguliwa kwa pamoja) na kwa Jina la Yesu Kristo aliweza kutembea pale pale hakika Yesu Kristo anaendelea kutenda hata sasa.
Hapa akionyesha kuwa maumivu yamemwacha kabisa akitembea bila ya maumivu.
Prophet Joseph akiwa na Venitha .
Venitha akishuhudia matendo makuu Mungu aliyomtendea.
Mama yake Venitha akishuhudia matendo makuu ya Mungu.
Hivi ndivyo mguu wa Venitha ulivyokuwa kabla ya maombi. Utukufu kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 2. Erick Maroba alikuja akiwa hana nguvu katika miguu yake lakini mara Prophet Joseph alipoongoza maombi ya kukataa kila aina ya ugonjwa ndugu Erick alisikia nguvu miguuni mwake na akaweza kutembea bila ya msaada wa gongo.
Akishuhudia jinsi alivyopokea uponyaji wa miguu yake.
Ndugu Erick akitembea bila ya kutumia gongo. Hakuna jambo gumu la kumshinda Mungu.