Dada yetu Jaquline Kaaya alipata neema ya kupokea neno la kinabii kutoka kwa Prophet Joseph, mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alimweleza kuwa mara nyingi dada huyu amekuwa akiota anahesabu fedha nyingi na mara kwa mara amekuwa akipoteza fedha katika mazingira yasiyoeleweka dada Jaquline akakiri kuwa hakika ni kweli ndipo mtumishi wa Mungu Prophet Joseph akamwambia kuanzia sasa hatapoteza hela tena na ameshuhudia ni kweli toka apate neno hilo la kinabii hajapoteza tena pesa. Na pia aliendelea kushuhudia matendo makuu ambayo Mungu amemtendea alikuwa ana uvimbe kwenye ziwa lake lakini alipopita katika mstari wa uponyaji (prayer line) uvimbe ulipotea kwa jina la Yesu Kristo na ni mzima kabisa.
Jaquline Kaaya akishuhudia jinsi Mungu alivyomtendea. UTUKUFU KWA YESU KRISTO WA NAZARETH.
No comments:
Post a Comment