TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 7 September 2014

UPONYAJI WAKATI WA PRAYER LINE.

Kila jumapili katika mstari wa uponyaji  (Prayer Line) tumeendelea kuuona ukuu na utukufu wa Mungu kupitia Prophet wake Prophet Joseph,maelu ya watu wamekuwa wakiponywa haijalishi ni ugonjwa wa aina gani, kuna waliokuja na Ukimwi,Kansa,Kisukari,Presha,Ulemavu na magonjwa mengine mengi lakini tumeshuhudia Yesu Kristo akiwaponya na kuwafungua na kuwa huru kabisa.



Kaka yetu Nisamba Aginom kutoka Congo aliweza kupata neema ya unabii kutoka kwa Mungu kupitia Prophet Joseph kuwa kila akienda kuoga mwili wake hutetemeka mara anagusa maji na ndio chanzo cha biashara zake kutokwenda vizuri naye akakiri kuwa ni kweli tupu.
                       Hapa prophet Joseph akimfungua kwa jina la Yesu Kristo.

                                            Akiwa chini kwa nguvu ya Mungu.
           Prophet Joseph akionyesha upendo wa kumfuta kaka yetu mara baada ya kufunguliwa.
                           Hapa Prophet Joseph akimkumbatia kaka yetu ikiwa ni ishara ya upendo.


 Mama yetu Dotto Fabian alikuja na tatizo la mguu, ansema lilianza kama muwasho alikuwa na muwasho kwenye mguu ghafla mguu ukaanza kuvimba na kujaa usaha na akawa hawezi kuembea .
 Kama mguu unavyoonekana hapa, lakini mara baada ya maombezi maumivu yote yakamwacha na akaweza kutembea na kukimbia bila ya kuwa na maumivu.

                                   Hapa akimshukuru Mungu kwa kumponya.

         Ndugu yetu Jige Mafuru alipata ajali ya pikipiki na kusababisha mguu wake kuvunjika mara mbili.


                                     Hapa akionekana mguu ukiwa na vyuma.

Hapa Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph akiamuru uzima kuingia katika mguu wa ngugu yetu.
                  Hapa akisimama mara baada ya roho ya ajali na maimivu kumwacha.

                       Hakuna jambo gumu la kumshinda Mungu. Yanayoshindikana kwa wanadamu kwake yanawezekana.

No comments:

Post a Comment